Thursday, February 6, 2014

MENEJA wa klabu ya Arsenal, Arsene Wenger ameondoa uwezekano wa kumsajili Luis Suarez kutoka Liverpool katika majira ya kiangazi baadae mwaka huu. Arsenal walijaribu kumsajili nyota huyo wa kimataifa wa Uruguay wakati wa usajili msimu uliopita huku Suarez mwenyewe akitaka kuondoka Anfield. Lakini Wenger amekanusha tetesi mpya zilizozuka kuwa bado wanahitaji huduma ya nyota huyo ambaye yuko katika kiwango cha juu msimu huu. Wenger amesema uhamisho wa mara ya kwanza wa Suarez haukufanikiwa hivyo mchezajihuyo hajawahi kuwa wa kwao na itabakia hivyo. 
 
Suarez mpaka sasa amefanikiwa kufunga mabao 23 katika mechi 19 alizoichezea 
Liverpool na kuwawezesha kuwepo katika nafasi nne za juu kwenye msimamo wa Ligi Kuu nchini Uingereza. Arsenal wanatarajiwa kukwaana na Liverpool katika Uwanja wa Anfiled Jumamosi ambapo wanaweza kuongeza pengo la alama kufikia 11 kama Daniel Sturridge of Liverpool is congratulated by teammates after scoring his team's third goal

0 maoni:

Post a Comment

waliotembelea blog