TIMU ya Vijana ya Mpira wa Miguu
ya Que Bac ya Mbagala Kipati jijini Dar es Salaam jana imeibuka bingwa
wa Mashindano ya Mbagala Cup baada ya kuibugiza timu ya mpira wa miguu
ya Kipati magoli 2 kwa bila. Que Bac imetawazwa mabingwa na kukabidhiwa
Mbuzi, seti moja ya jezi pamoja na mpira.
Que Bac ndio waliokuwa wa kwanza
kuzifumania nyavu za Kipati ndani ya dakika 45 za kipindi cha kwanza
ambapo mshambuliaji wao hatari, Yahya Tumbo (9) alikwamisha mpira katika
nyavu za wapinzani baada ya kuunganisha pasi kutoka kwa mchezaji
mwenzake. Lakini hadi kipindi cha kwanza kinamalizika Que Bac walikuwa
mbele kwa goli moja.
Kipindi cha pili kilianza kwa kasi
ambapo wachezaji wa Kipati waliongeza mashambulizi kwa wapinzani wao
kutaka kusawazisha goli lakini goli kipa wa Que Bac pamoja na walinzi
wake walikuwa makini na kuondoa hatari zote mara kadhaa langoni mwao.
Jahazi la Kipati lilizamishwa
zaidi na mshambuliaji wa Que Bac, Shine Duu jezi namba 17 ambaye
alifanikiwa kuifungia timu yake goli la pili na kuongeza matumaini ya
kutangazwa Mabingwa wa Mashindano hayo (Mbagala Cup). Hadi kipenga cha
mwisho Que Bac 2 na Kipati 0.
Akizungumza mara baada ya mchezo
wa fainali, Mratibu wa Mashindano hayo, Musa Hemed (Kibwetele) alisema
mashindano hayo yalianza rasmi Aprili 5, 2014 ambapo timu 16 zilishiriki
katika mashindano huku zikiwa katika makundi mawili, yaani A na B na
kila kundi lilikuwa na timu nane. Alisema mshindi wa pili katika
mashindano hayo amefanikiwa kupata seti moja ya jezi pamoja na mpira,
huku zawadi mbalimbali zikitolewa kwa wachezaji na timu yenye nidhamu.
Alisema lengo la mashindano hayo
ilikuwa kuwakuza vijana katika vipaji vyao kwenye fani ya mpira wa miguu
pamoja na kuwaunganisha vijana kushiriki katika michezo kwa pamoja.
“…Sisi eneo letu tumezoea kuona mashindano ambayo yanaanzishwa labda na
diwani lakini tena mara moja kwa muda mrefu. Sasa mimi nikakaa na
kufikiria nasie vijana tunaweza kujipanga na kuanzisha mashindano kama
hayo,…nikazialika timu tukachangishana ada kidogo na hatimaye tukapata
mlezi wa mashindano na yamefanyika,” alisema Kibwetele.
Akizungumza mara baada ya
kukabidhi zawadi, mgeni rasmi katika fainali hizo alikuwa ni Kaimu
Mkurugenzi wa Teknolojia na Mawasiliano Mamlaka ya Bandari (TPA) ambaye
pia Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM, Temeke (MNEC), Phares Magesa
ameahidi kuyafadhili mashindano hayo kuanzia sasa na atakuwa akiwezesha
kufanyika kwake.
Mbali na kiongozi huyo kuyafadhili liongeza zawadi kwenye mashindano hayo ambapo alitoa shilingi laki moja moja kwa mchezaji bora, kipa bora na waamuzi na kamati ya maandalizi wa mashindano hayo.
Mbali na kiongozi huyo kuyafadhili liongeza zawadi kwenye mashindano hayo ambapo alitoa shilingi laki moja moja kwa mchezaji bora, kipa bora na waamuzi na kamati ya maandalizi wa mashindano hayo.
Naye Mlezi wa Mashindano hayo,
Emmanuel John alisema lengo la mashindano hayo ni kutaka kuwaleta vijana
karibu, kuleta upendo dhidi yao na kudumisha umoja na amani kwa vijana
wote. Alisema mashindano kama hayo yanawatoa vijana kutoka katika
mtizamo ya wao kukaa vijiweni na kujishughulisha na michezo zaidi ambayo
inamanufaa kwao kuliko kushinda wakipiga soga kwenye makundi vijiweni.
Zimeshiriki Kata tano za Kata ya Mbagala, Kata ya Kiburugwa, Kata ya
Kijichi, Mbagala Kuu
“Unajua vijana wengi mitaa yetu
wanakaa vijiweni si kwamba wanapenda kufanya hivi, wanafanya tu
kwasababu wanakosa cha kufanya…sasa kuna kila sababu watu wenye nafasi
kujitokea na kuwawezesha ili kuwatoa walipo, nimetokea mimi nimedhamini
mashindano yamefanyika, wameshindana na vijana wamepata burudani, upendo
na amani pia mshindi kapatikana,” alisema.
Aidha alisema wapo vijana wengi
wenye vipaji ambao wanaitaji kupewa nafasi za kushiriki katika
mashindano kama hayo na hatimaye vipaji vyao kuonekana na kuendelezwa
katika mashindano ya juu. “…Tumeona leo hapa vijana wameondoka na zawadi
mbalimbali wachezaji bora wamezawadiwa, timu bora, golikipa bora
kapatikana, timu zimejishindia jezi na mipira vyote vyao…timu hizi awali
zilikuwa zikicheza na jezi za kukodisha lakini leo wamepata za kwao
baada ya kushinda,” alisema.
Kijana huyo alisema anajivunia
kuwa sehemu ya kupunguza maovu kwa vijana kwani katika kipindi chote cha
mashindano hayo vijana walielekeza nguvu zao nyingi kwenye michezo
kimashindano jambo ambalo anaamini limepunguza baadhi wenye nia ovu
kubadili mienendo yao kutokana na mashindano hayo. Pamoja na hayo
aliishauri Serikali na vyama vya soka kushuka ngazi ya chini mitaani
kusaka vipaji vya michezo anuai kwani zipo vingi lakini vinakosa fursa
ya kuonekana.
0 maoni:
Post a Comment