Sunday, August 10, 2014

IMG-20140809-WA009
Timu ya Kivule veterani ya jijini Dar es salaam kwenye picha ya pamoja kabla ya kuvaana na timu ya Namanga veteran kwenye uwanja wa Sheikh Amri Kaluta Abeid jijini Arusha
Mahmoud Ahmad Arusha
Timu ya Ushirika Veteran ya mkoani Kilimanjaro imeibuka bingwa wa Bonanza la Nanenane kwa kuifunga timu ya Kivule veteran ya ukonga jijini Dar es salaam kwa magoli 3-0  katika mchezo wa fainali ya mashindano hayo yaliondaliwa na timu ya Arusha All Stars kwenye uwanja wa sheikh Amri Abeid jijini Arusha.
 
Michezo hiyo ya nanenane iliyozishirikisha timu kutoka mikoa ya Arusha,Dodoma, Mwanza,Dar es salaam na Kilimanjaro ambao timu yao ndio waliibuka mabingwa wa mashindano hayo kwa timu za ushirika veteran na kivule kucheza fainali
 
Hata hivyo wenyeji wa mashindano hayo waliambulia nafasi ya nne baada ya kufungwa katika mechi ya kugombea nafasi ya tatu na timua ya Dodoma veteran iliyokuwa inaongozwa na mkongwe wa soka hapa nchini Charles Mgodo.
 
Akizungumza baada ya mechi hiyo mgodo aliwataka wachezaji wa sasa kuangalia michezo ya maveterani katika mabonanza mbalimbali kwani watajifunza kitu kutoka kwao ikiwemo nidhamu ya michezo na kujituma kama walivyoonyesha baadhi ya wachezaji wa miaka ya nyuma wa timu zilizotamba kwenye ligi kuu.
 
Pia Mgodo alisema kuwa maandalizi ya timu za vijana wa sasa na wazamani ni tofdauti huku akisema kuwa vijana wa sasa wanataka kucheza kama mchezaji Fulani baada ya kuangalia tv huku hawajitumi hili ni tatizo na kuwataka kuanza kujituma na kutoweka maslahi mbele na kuuvaa uzalendo.
 
Akalishauri shirikisho la michezo hapa nchini Tff kurudi mashuleni au kuanzisha Academy ilkuweza kuibua vijapaji na sio kuviacha vikielea bila ya kuviendeleza hili ni tatizo kwa ukuaji wa michezo hapa nchini.
 
“Tunataka vijana wakija kwenye mabonanza waje kujifunza mpira na kuangalia tofauti ya mpira wanaocheza wao na wa wazee wao hapa umeona wachezaji wa zamani wakijituma tokea mwanzo wa mchezo hadi mwisho na wao wanatakiwa kuwa kama hivi ila kikubwa wawe wazalendo kwa taifa lao hapo tutafanikiwa”alisema Mgodo.

0 maoni:

Post a Comment

waliotembelea blog