Tamasha la Mwanamuziki mkongwe wa nyimbo za asili nchini Saida Karoli limefana usiku huu kwenye ukumbu wa Lina's Night Club Bukoba. Tamasha lililokuwa linaitwa "usiku wa Saida Kaoli" huku watu wengi wakijitokeza kumuona kwa mara ntingine hapa Bukoba Tangu azushiwe na wadau kwamba alifariki Dunia katika ajali ya boti miezi michache iliyopita habari iliyokuwa ya uzushi mtupu na ya uhongo. Leo hii jumamosi akiwa amesindikizwa na wasanii wa hapa Nyumbani Bukoba Bk Sande, Papaa Kishaju, wanamuziki wa VISION MUSIC AMBASSADOR wanaodhaminiwa na 100.0 Vision fm Radio BUKOBA na Kundi la Ka Jay Poda kutoka Kenya wameusindikiza usiku wa SAIDA KAROLI vilivyo na kukamua kisawasawa kwenye ukumbi LINA'S usiku huu. 
Saida Karoli akiimba baadhi ya nyimbo zake mpya

Willy Kiroyera kulia akicheza na Saida Karoli

Saida karoli mizuka ikimpanda

Baadhi ya wageni rasmi meza kuu kushoto ni Afisa Utamaduni

Ilifika nafasi ya msanii wa kizazi kipya BK Sande nae akapanda kwenye steji kuporomosha nyimbo zake kuwaburudisha mashabiki wake ukumbini.

Bk Sande mtoto wa Nyumbani akiendelea kuimba

Bk Sande

Kulia Mkuu wa Chuo cha KCC Bw. Subira na mkewe wakiburudishwa hapa na wanamuziki wa hapa Nyumbani


Saida na Wanamuziki wake wakiendelea kuimba

Ukumbi ukiburudika vilivyo usiku huu

Saida akiimba

Kweli bado jembe saida!!

Usiku wa Saida na Saida akiutendea haki hapa!!

Baadhi ya wadau waliojitokeza usiku huu

Saida Karoli akiendelea kuburudisha

Kundi ka Ka jay Poda kutoka Kenya likitumbuiza ukumbini

Tanzania safii...Raha ya Nyumbani, angalia na wazungu nao wapo wakiburudishwa.

Kiongozi wa kundi la ka jay poda!! kutoka kenya akikata mauno usiku huu

Kiongozi wa kundi la ka jay poda!! kutoka kenya

Wadau mbalimbali

Bw. Muganyizi

Kulia ni Mgeni Rasmi Afisa Utamaduni na kushoto ni mwandaaji wa Tamasha hili ambaye ni mkuugenzi wa Tivol Studio ya jijini Mwanza.

Wageni Rasmi.

Bw. Willy O Rutta ( Kiroyera) kulia na Bw. Ernest Nyambo wakicheki kisawasawa burudani

Dada akibaki mdomo wazi huku akiwa aamini macho yake kwa kile alichoburudishwa kutoka kwa msanii mkongwe Saida Karoli.

Kila mtu hapa alitamani kusimama na kucheza maana nyimbo zenyewe zilihamasisha kucheza

Chezea Saida wewe!!

Usikubali kupitwa na wakati!!!

Dada ilibidi wanyanyuke na wamsogelee Saida huku ngoma ikicharazwa na Saida mwenyewe!!

Wakati ndio huu!!!
Kesho Jumapili Tarehe 8.9.2013 Saida ataendelea kwenye tamasha la pili katika uwanja wa Kaitaba Kiingilio ni Tsh.2500/= tu. Saida Karoli atasindikizwa na Jopo la wasanii lukuki waliowahi kurekodia nyimbo zao ndani ya Tivol Studio wakiwemo wasanii wa nchi Jirani na wa hapa nyumbani Bukoba.
Hapa umefika!!

Ni yeye kweli au!!

Hapa ni nyumbani kukamua lazima!!1

wewe!!eee

Dada akitokelezea kwenye jicho la kamera

Wadau. kulia ni Bw. jamal kurumuna
0 maoni:
Post a Comment