Wednesday, October 22, 2014

NeymaJr aliendeleza tabia yake ya kufunga, huku Lionel Messi akiendelea kushindana na Cristiano Ronaldo katika orodha ya kuwania ‘ heshima ya mfungaji bora wa muda wote’ wa ligi ya mabingwa Ulaya. Messi pamoja na Ronaldo wamebakiza mabao mawili mawili kila mmoja ili kufikia rekodi ya muda mrefu ya mabao 69 ambayo inashikiliwa na mshambulizi wa zamani wa Hispania na klabu ya Real Madris, Raul Gonzalez Blanco.
Barcelona ilifanikiwa kuchomoza na ushindi wa pili msimu huu baada ya kupoteza mchezo dhidi ya vinara wa kumdi hilo, PSG wiki tatu zilizopita. Ushindi wa usiku wa jana dhidi ya Ajax umewafanya mabingwa hao wa zamani kufikisha pointi sita, pointi moja nyuma ya mabingwa wa Ufaransa ambao walishinda ushindi mwembamba dhidi ya Apoel Nicosia katika uwanja wa Neo GSP Stadium, shukrani kwa bao la dakika ya 87 kutoka kwa Edson Cavani.
Anwar El-Ghazi aliwafungia Ajax bao la kufutia machozi katika dakika ya 88 lakini kinda Sandro Ramirez ambaye aliingia kuchukua nafasi ya Neymar alifunga bao la tatu kwa wenyeji na kutengeneza ushindi wa mabao 3-1 katika dimba la Camp Nou

0 maoni:

Post a Comment

waliotembelea blog