Didier Drogba alifunga bao
lake la kwanza katika kikosi cha Chelsea. Drogba mara ya mwisho
aliifungia Chelsea katika mchezo wa fainali wa michuano hiyo dhidi ya
Bayern Munich miaka miwili iliyopita. Akiingia uwanjani kuchukua nafasi
ya Loic Remy aliyeumia katika dakika ya 16, Drogba alifunga kwa mkwaju
wa penalti dakika saba baadae. Chelsea ilichomoza na ushindi wa kishindo
wa mabao 6-0 dhidi NK Maribor.
Remy alifunga bao la kuongoza katika uwanja wa Stamford Bridge katika dakika ya 13, nahodha, John Terry alifunga bao tatu katika dakika ya 31 na kufanya wenyeji kupumzika wakiwa na mabao 3-0. Mlinzi wa Maribor, Mitja Viler alijifunga katika dakika ya 54, EDem Hazard akafunga kwa mkwaju wa penalti zikiwa zimesalia dakika 13 mchezo umalizike na Hazard akarudi kwa mara nyingine kuhitimisha ushindi wa Chelsea kwa bao la dakika ya mwisho ya mchezo.
Katika mchezo mwingine wa kundi hilo, mshambulizi, Maxim Choupo-Moting alifunga bao la ushindi katika mchezo ambao ulitoa mabao saba. Wenyeji, Svhalke 04 waliduwazwa na bao la mapema la kiungo-mshambulizi, Nani. Chinedu Obasi aliwafungia wenyeji bao la kusawazisha na kufanya hadi mapumziko ubao wa matokeo kusoma ‘ FC Schalke 1-1 Sporting Lisbon.
Wageni walicheza pungufu kwa dakika 60 baada ya kiungo ,Mbrazil, Mauricio Dos Santos Nascimento kuondoshwa uwanjani kwa kasi nyekundu katika dakika ya 33. Mshambulizi, Klans Jan Huntelaar aliwafungia wenyeji bao la pili dakika tano bsaada ya kuanza kwa kipindi cha pili, mlinzi Benedikt Howedes alifunga bao lingine katika dakika ya 60 lakini Sporting walirudi kwa kasi wakiwa pungufu na kufunga bao la mkwaju wa penalti kupitia kwa Adrien Silva dakika nne baada ya Schalke kufunga bao la tatu.
Raia huyo wa Brazil alifunga bao lingine dakika ya 78 na kutengeneza matokeo ya 3-3 kabla ya kupoteza mchezo huo dakika ya mwisho. Kwa matokeo hayo, Chelsea Chelsea wanaongoza kundi hilo wakiwa na pointi saba, wakifuatiwa na Schalke 04 wenye pointi tano, Maribor wanashika nafasi ya tati wakiwa na pointi mbili wakati Sporting wanaburuza mkia wakiwa na pointi moja. Kila timu I,echeza michezo mitatu.

0 maoni:
Post a Comment