TAYARI mchakato wa uchaguzi
katika klabu ya Simba sc umeshaanza na tayari mwenyekiti wa kamati ya
uchaguzi, Damas Ndumbaro ametangaza kuwa juni 29 mwaka huu uchaguzi
utafanyika
Wapo watu wengi wanaotamani kuiongoza klabu ya Simba ambayo kwasasa ipo katika hali ngumu kwa soka la uwanjani.
Kumaliza nafasi ya nne nyuma ya Mbeya City, Yanga na Azam fc ni jambo linalowaumiza wana Simba wote.
Ni msimu wa pili mfufulizo Simba
wanakosa nafasi ya kushiriki michuano ya kimataifa. Kwa ukongwe wake ni
jambo la fedheha kubwa japokuwa mpira uko hivyo.
Hatuwezi kuwakosoa Simba kwa
matokeo waliyokuwa wanapata kwasababu mpira wa miguu huwa unabadilika,
lakini makosa yanapotokea kwasababu ya watu fulani kutowajibika, hapo
lazima ukosoaji uhusike.
Kwa mfano wachezaji kushindwa
kucheza vizuri kwasababu hawajalipwa posho na mishahara, unashindwaje
kuukosoa uongozi kwa kushindwa kuwajibika?
Kumekuwapo na mivutano ya muda
mrefu baina ya mwenyekiti wa Simba, sasa Rais, Ismail Aden Rage
na baadhi ya wajumbe wake wa kamati ya utendaji pamoja na baadhi ya
wanachama.
Sinema nyingi zimeonekana na zimeandikwa, kila mtu anafahamu yaliyokuwa yanatokea Simba sc
0 maoni:
Post a Comment