Thursday, May 8, 2014


WACHEZAJI maarufu wa Klabu ya AC Milan ya Italy, Kaka na Robinho, sasa ni rasmi hawatacheza Timu ya Taifa ya Brazil kwenye Fainali za Kombe la Dunia zinazoanza kuchezwa Nchini Brazil kuanzia Juni 12 hadi Julai 13 baada Kocha wa Brazil, Luiz Felipe Scolari', Leo kutangaza Kikosi chake cha awali cha Wachezaji 23.
Pamoja na hao wawili pia hawamo Mkongwe Ronaldinho na Winga wa PSG, Lucas Moura.
Wachezaji wanne wa Chelsea, David Luiz, Oscar, Ramires na Willian, wote wamo ila Viungo wawili wa Liverpool, Philippe Coutinho na Lucas Leiva, wamekosa namba, huku Paulinho wa Tottenham na Fernandinho wa Man City, wakiwemo kundini.
Brazil reveal World Cup squad as Kaka, Robinho and Lucas Moura miss out
Brazil, pamoja na Nchi nyingine zote zinazocheza Fainali, zinapaswa kusajili Vikosi vyao vya Wachezaji 23 kwa FIFA ifikapo Juni 2.
Brazil, ambao kwenye Fainali za Kombe la Dunia wapo KUNDI A pamoja na Croatia, Mexico na Cameroon, watacheza Mechi ya Kirafiki na Panama Juni 3 huko Golania, Brazil na kisha Juni 6 kuivaa Serbia huko Sao Paulo, Brazil.
Brazil watafungua rasmi Kombe la Dunia hapo Juni 12 kwa kuivaa Croatia katika Mechi ya KUNDI A.


KIKOSI KAMILI:
MAKIPA:
Julio Cesar (Toronto FC, Mkopo toka QPR), Jefferson (Botafogo), Victor (Atletico Mineiro).
MABEKI: Marcelo (Real Madrid), Daniel Alves (Barcelona), Maicon (AS Roma), Maxwell and Thiago Silva (both Paris St-Germain), David Luiz (Chelsea), Dante (Bayern Munich), Henrique (Napoli).
VIUNGO: Paulinho (Tottenham Hotspur), Ramires (Chelsea), Willian (Chelsea), Oscar (Chelsea), Hernanes (Inter Milan), Luiz Gustavo (Wolfsburg), Fernandinho (Manchester City).
MAFOWADI: Bernard (Shakhtar Donetsk), Neymar (Barcelona), Fred (Fluminense), Jo (Atletico Mineiro), Hulk (Zenit St Petersburg).


RATIBA:Mechi za Ufunguzi:
Alhamisi 12 Juni 2014
KUNDI A
23:00 Brazil vs Croatia
Ijumaa 13 Juni 2014
19:00 Mexico V Cameroon

0 maoni:

Post a Comment

waliotembelea blog