Jose
Mourinho anaweza kuwa kocha wa nne kumaliza msimu bila kombe kwa klabu
ya Chelsea tokea Roman Abramovich aanze kuimiliki klabu hiyo. Alianza
Claudio Ranieri kukosa kombe akafukuzwa kazi akifuatiwa na Carlo
Ancelotti na Avram Grant. Hadi sasa klabu ya Chelsea imeshatolewa kwenye
michuano yote ya ndani na nje ya England huku ikiwa nafasi ya tatu
kwenye ligi kuu. Ni wazi kuwa Chelsea haitaweza kushinda kombe la ligi
kuu na hivyo kumfanya Mourinho kumaliza msimu bila kombe lolote. Lakini
hadi sasa hakuna fufunu zozote kuwa Mourinho atafukuzwa kazi kutokana na
ugeni wake ndani ya klabu baada ya kurudi akitokea Madrid. Ukweli ni
kwamba Mourinho ataendelea kuifundisha Chelsea kwa msimu mwingine zaidi
ili kuirudisha klabu tena Chelsea kwenye kiwango chake kilichozoeleka.
Tatizo kubwa la klabu ya Chelsea msimu huu lilikuwa ni safu ya
ushambualiji na tayari Mourinho ameshaonesha nia ya kumsajili Diego
Costa (Atl. Madrid) baada ya kushinda kumnasa Rooney.
0 maoni:
Post a Comment