Monday, September 22, 2014


Steven Gerrard looked out of sorts in Liverpool's disappointing 3-1 loss against West Ham on Saturday
Steven Gerrard alionekana mweny huzuni baada ya kuchapwa 3-1 na West Ham 

BRENDAN Rodgers ametetea kiwango cha Steven Gerrard, akisisitza kuwa nahodha huyo mkongwe wa Liverpool hahitaji kupumzika zaidi.
Gerrard mwenye miaka 34, amecheza kila dakika msimu huu, zikiwemo mechi tatu katika wiki na kushuhudia Liverpool akipoteza michezo miwili ya ligi kuu mbele ya  Aston Villa na West Ham.
Pia alicheza na kufunga penalti katika mechi ya ligi ya mabingwa dhidi ya wakali wa Bulgaria, Ludogorets.
Rodgers  na wasaidizi wake wanafahamu kuwa katika mechi zote za ligi kuu Gabriel Agbonlahor na Stewart Downing walifanikiwa zaidi na kumzidi kete Gerrard ambaye alishindwa kugawa mipira kama alivyozoeleka.
Reds manager Brendan Rodgers hands out instructions to his skipper from the sidelines at Upton Park
Kocha wa wekundu wa Anfield, Brendan Rodgers akimpa maelekezo nahodha wake katika uwanja wa  Upton Park
Liverpool host Middlesbrough on Tuesday in the Capital One cup, with Grant Leadbitter (left) in great form for the North East club
Liverpool wataikaribsiaha Middlesbrough leo jumanne katika mechi ya  Capital One cup, ambayo itamtumia nyota wake  aliye katika kiwango cha juu, Grant Leadbitter (kushoto) 


Nahodha huyo wa zamani wa England alikosea pasi 11 dhidi ya West Ham katika kipindi cha kwanza na alishindwa kumiliki mpira mara 14.
Rodgers alikuwa na mipango ya kumpumzisha Gerrard wakati Liverpool inacheza mechi ya Capital One leo dhidi ya Middlesbrough, lakini kila kitu kimevurugika baada ya Jordan Henderson na Philippe Coutinho kupata majeruhi.
Alipoulizwa kiwango cha nahodha wake jana, Rodgers alisema: "Hakuna tatizo. Ni mchezaji muhimu kwetu. Kiwango cha timu hakikuwa kizuri. Tumejitahidi kuimarisha kiwango chake kwa misimu miwili iliyopita na wakati huo alikuwa anacheza soka la kimataifa. Ukiangalia idadi ya mechi alizocheza, amekuwa mzuri sana".
"Yupo katika umri ambao tunatakiwa kumtunza yeye binafsi. Tunamtaka kuhusika katika mechi kubwa kwasababu ya uzoefu wake na siku zote tutafanya kila linalowezekana kumfanya awe bora"
"Tutawafahamisha kama atapumzishwa. Baadhi ya wachezaji vijana watahusishwa katika kikosi".

0 maoni:

Post a Comment

waliotembelea blog