Monday, September 22, 2014


Leicester City wameifunga Manchester United bao 5-3 kwenye uwanja wao wa nyumbani King PowerRobin Van Persie na Di Maria ndio wameifungia bao United kipindi cha kwanza..Di Maria akishangilia bao lake la pili kwa United ugenini huko King PowerKipindi cha kwanza dakika ya 13 Robin Van Persie anaipachikia bao la kichwa Manchester United baada ya kuunganisha krosi safi kama kona kutoka kwa Radame Falcao.
Dakika ya 16 Ángel Di María alipachika bao la pili na kufanya 2-0 lakini nao Leicester walipata bao lao nao dakika ya 18 kupitia kwa L. Ulloa bao la kichwa baada ya kupata ushirikiao kutoka wa krosi kkutoka kwa  Jamie Vardy na kufanya 2-1.Leicester nao walifanikiwa kufunga bao lao dakika ya 18 kupitia kwa José Ulloa.
 Kipindi cha pili dakika ya 57 Ander Herrera alipachika bao la tatu muda punde nao  Leceister walipatabao la pili kupitia penati ya utata na kufanya 2-3 mkwaju uliopigwa na D. Nugent katika dakika ya 62.
Dakika ya 64 E. Cambiasso aliwasawazishia bao kwa kufanya 3-3 Leceister City.
Jamie Vardy aliwachapa bao la nne na kufanya 4-3 baada ya kuwatoka mabeki wa United na kutupia baada ya kutanguliziwa mpira na Ritchie De Laet. bao la tano lilifungwa kwa mkwaju wa penati tena kupitia kwa José Ulloa dakika ya 83.

VIKOSI:Leicester: Schmeichel, De Laet, Morgan, Moore, Konchesky, Cambiasso, Nugent, Drinkwater, Hammond, Vardy, Ulloa.
Akiba: James, King, Hamer, Schlupp, Mahrez, Wasilewski, Wood.

Manchester United: De Gea, Da Silva, Evans, Blackett, Rojo, Blind, Ander Herrera, Di Maria, Rooney, Falcao, Van Persie.
Akiba: Shaw, Mata, Januzaj, Smalling, Lindegaard, Fletcher, Valencia.
Refa: Mark Clattenburg

0 maoni:

Post a Comment

waliotembelea blog