5
Jose Mourinho anasema mapenzi ya Frank Lampard kwa Chelsea yalikwisha baada ya kujiunga na washindani wake
JOSE Mourinho amesema mapenzi ya Frank
Lampard kwa Chelsea yamekwisha baada ya jana kuifungia Manchester City
bao la kusawazisha katika dakika za majeruhi uwanja wa Etihad.
Nyota huyo mwenye rekodi ya kufunga
mabao mengi kwa muda wote Chelsea, alitokea benchi na kuiadhibu timu
yake hiyo ya zamani, lakini Mourinho aligoma kukubali kuwa mchezaji huyo
anayecheza kwa mkopo Man City ana mapenzi ya kweli kwa Chelsea.
Alisema: "Frank ni mchezaji wa Man City, siamini hadidhi zake na mapenzi ya moyoni kwake, labda mimi ni mshamba wa mpira"
5
Lampard akiteleza katika eneo la penalti na kuifungia City bao.
"Alipoamua kwenda kwa washindani wa moja kwa moja na Chelsea, mapenzi kwa timu yalikwisha. Alifanya kazi yake kiuweledi.
"Alipokelewa vizuri England na hii ndio
England na hii ndio Chelsea. Watu wa Chelsea kamwe hawasahau kile watu
wa Chelsea walifanya".
"Iliwahi kunitokea hata mimi nikiwa kocha wa Inter. Ni utamaduni na uzuri wa Chelsea".
0 maoni:
Post a Comment