Friday, September 19, 2014


MBALI ya Wachambuzi kukuna vichwa jinsi Louis van Gaal atakavyopanga Kikosi chake kipya kilichosheheni Majina makubwa, ‘Galacticos’ kama walivyobatizwa hivi sasa huko Uingereza, sasa pia kumeibuka mjadala mwingine nani atatwishwa zigo la kupiga Frikiki wakati wa Mechi za Manchester United.
Je ni Angel di Maria, Juan Mata, Wayne Rooney, Robin van Persie au Radamel Falcao?

Wote hao wana rekodi nzuri za kufunga Mabao kwa Frikiki kwa kuwa ni wapigaji stadi ya Mipira iliyokufa. 
Angel di Maria alichomoza vizuri kwenye Mechi iliyopita ambayo Man United waliichapa Queens Park Rangers Bao 4-0 Wikiendi iliyopita alipofunga Bao la kwanza kwa Frikiki safi sana.
Rooney curls home a free-kick in United's 2-0 win over Crystal Palace at Old Trafford last season
Lakini kila mmoja kati ya hao Watano ana uwezo mkubwa kufunga na Juan Mata amefunga Bao 4 kwa Chelsea na Man United tangu 2011 mbili zikiwa Msimu uliopita alipoifungia Man United kwenye Mechi dhidi ya Newcastle United na Southampton.. Robin van Persie curls home his stoppage time free-kick against Manchester City in 2012
Wayne Rooney amefunga Frikiki 5 katika Misimi Mitatu iliyopita na kwa vile yeye ndio Nahodha basi sauti kubwa itakuwa yake.
As captain, Wayne Rooney may be able to pull rank when it comes to taking free-kicks
Ingawa si Wafungaji wa mara kwa mara kwa Frikiki Robin van Persie na Radamel Falcao nao ni Wataalam wa Mipira hiyo.
Nani atatwishwa zigo la kupiga Frikiki ni juu ya Van Gaal na, pengine, Nahodha Wayne Rooney.
Mata akipiga frii kiki kwenye moja ya mechi zao.

0 maoni:

Post a Comment

waliotembelea blog