Tuesday, June 3, 2014

NA Mwandishi Wetu,Tanga.
Wasanii nguli wa mziki wa Bongo Fleva na Filamu ambao ni wazawa wa mkoa wa Tanga wanatarajiwa kushiriki kwenye Tamasha ya kuuchangia mfuko wa Klabu ya Coastal Union ya Tanga ambayo inajiandaa na Ligi Kuu msimu ujao.
Tamasha hilo litafanyika mapema mwezi Agosti mwaka huu baada ya kumalizika mwezi wa ramadhani na kabla ya ligi kuu Tanzania bara haijaanza.

Akizungumza jana Mratibu wa Tamasha hilo,Salim Bawaziri alisema lengo kuu lake ni kutaka kuwakutanisha wadau mbalimbali ikiwemo wana michezo,wasanii,wafanyabiashara na wabunge wa mkoa wa Tanga ili kuweza kuisapoti timu hiyo kwa ajili ya harakati zake za ligi kuu.
Bawaziri alisema asilimia kubwa ya kuelekea maandalizi yake yanaendelea vema ambapo mazungumzo yanaendelea baina ya wasanii watakaotumbuiza siku hiyo wakiwemo Waziri Njenje na Hamisi Mwinyuma “Mwana FA” na wengine wengi.
Aliwataja wasanii ambao wanatarajiwa kutoa burudani siku hiyo kuwa ni Matonya,Tanga Clan,Parklane,Wagosi wa Kaya,TNG Squard,Abubakari Katwila Q.Chief,Rashid Makwiro “Chid Benzi”Nassoro Hamisi “Best Naso”
Ibrahimu Mussa “Roma Mkatoliki” wakiwemo King Majuto ,Rose Ndauka na Tito na wengine wengi.

Mratibu huyo alisema katika kuhakikisha suala hilo linapata mafanikio aliwashirikisha wadau wengine kwa ajili ya maandalizi hayo wakiwemo Mohamed Bawaziri na kiongozi mmoja wa ngazi za juu serikali ambaye
hakupenda kuliweka jina lake bayana.

Alisema katika tamasha hilo wanatarajia kumualika Mke wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mama Salma Kikwete kuwa mgeni rasmi lengo likiwa ni kuhakikisha mfuko wa Coastal Union unakuwa na
mafanikio.

Aidha alieleza kwa kuwashirikisha wasanii hao pamoja na watu maarufu waliopo nje na ndani ya Tanga kushiriki kwenye tamasha hilo ili kuchangia misaada mbalimbali.

0 maoni:

Post a Comment

waliotembelea blog