Monday, August 10, 2015



Oxford alimkaba Mtu mzima Mesut Ozil wa Arsenal na aliyenunuliwa £42.5million leo jumapili kwenye Uwanja wa Emirates, West Ham wameshinda bao 2-0 dhidi ya Arsenal.
Chipukizi Reece Oxford wa West Ham ameweka rekodi kwa kuwa mchezaji mchanga zaidi wa saba na umri wa miaka 16.

Oxford alipumzishwa na Meneja mpya wa West Ham Slaven Bilic kipindi cha pili dakika ya 79.
Reece Oxford leo wakati anacheza na Wakongwe Arsenal
Leo ameweka Historia kwenye Uwanja wa Emirates alipoisaidia Timu yake West Ham kuifunga Arsenal Bao 2-0 katika Mechi ya kwanza ya Msimu mpya wa Ligi Kuu England kwa Timu hizo.
Reece anakuwa miongoni mwa Kijana mdogo kucheza Ligi Kuu England yeye akiwa na Miaka 16 na Siku 236 akiwa nyuma ya Mchezaji mdogo kabisa, Matthew Briggs, ambae alicheza Mechi yake ya kwanza kwa Klabu yake Fulham ilipofungwa 3-1 na Middlesbrough Mei 2007.
Siku hiyo, Briggs alikuwa na Umri wa Miaka 16 na Siku 65.
Oxford Reece alianzia Soka lake hapo hapo West Ham na Leo Meneja mpya Slaven Bilic alimpa nafasi ya kuanza Mechi hii ya Ligi dhidi ya Arsenal akicheza kama Kiungo Mkabaji mbele ya Difensi yake ya Mtu 4 akimudu kuwakalisha Mastaa kina Santi Cazorla, Mesut Ozil na Olivier Giroud.

Reece alicheza Mechi hiyo kwa Dakika 79 hadi alipobadilishwa na kuingizwa Mkongwe Kevin Nolan ambae ni mkubwa wake kwa Miaka 17.
Kinda huyo, mwenye Urefu wa Futi 6 na Inchi 3, kama ingekuwa Afrika bila shaka Watu wangetilia wasiwasi umri wake lakini Meneja wake, Bilic, ameeleza: “Kama Messi angekuwa mbele yangu ningekuwa na mchecheto lakini si yeye.”
Bilic aliongeza: “Watu wananiuliza: ‘Una hakika ana Miaka 16?’ Ni hatari kumchezesha lakini niliamini ana uwezo. Nasikia fahari kwake. Kwenye Karatasi tu ndio ana Miaka 16. Huyu ni sehemu ya kizazi hiki kipya!”
Nae Mchezaji mwingine mzoefu wa West Ham, Winston Reid, amesema: “Ni Kijana mdogo wa Miaka 16 lakini ana umbo kubwa kupita mie! Pengine ana uwezo Zaidi kupita mie!”
Hata Meneja wa Arsenal, Arsene Wenger, ameungama kuwa Reece Oxford ni Kijana Jembe.

0 maoni:

Post a Comment

waliotembelea blog