Monday, August 10, 2015



Full time, Arsenal 0 vs 2 West Ham United
Meneja mpya Slaven Bilic ameanza Ligi Kuu England kwa kuiongoza Timu yake West Ham kuitandika Arsenal 2-0 kwenye Dabi ya Jiji la London huko Emirates na kumfanya Meneja wa Arsenal Arsene Wenger kutoamini kilichomkuta na kubaki kushika kichwa, West Ham, ambao walimchezesha Kijana wa Miaka 16 Reece Oxford, walifunga Bao lao la kwanza baada ya Kipa wa Arsenal Petr Cech kuitokea Frikiki na kuikosa na kumruhusu Cheikhou Kouyate kufunga kwa kichwa katika Dakika ya 43.
Nafasi pekee waliyokaribia Arsenal kufunga katika Kipindi cha Kwanza ni pale Aaron Ramsey alipopiga Posti.

Zarate dakika ya 57 aliwachapa bao la pili Arsenal na kuipa bao la pili West Ham dhidi ya Wenyeji wao Arsenal kwenye Uwanja wa Emirates na kufanya Gunners wachanganyikiwe na kumuingiza Alexis Sanchez ili awaokoe lakini mambo yakaenda kombo.Bao la West Ham lilifungwa kipindi cha kwanza dakika ya 43 kupitia kwa Cheikhou Kouyaté alipolifunga kwa kichwa kupitia mpira wa adhabu uliopigwa na Dimitri Payet na kisha Cheikhou Kouyaté kuunganisha vyema hadi langoni mwa Arsenal.Santi Cazorla akilindwa na msitu wa West Ham United katika kipindi cha kwanza.

0 maoni:

Post a Comment

waliotembelea blog