Monday, August 10, 2015



Kepteni wa Lazio ya Italy Lucas Biglia ameafika Mkataba wa Miaka Minne Klabu hiyo ya England.
Ripoti hizo, ambazo chanzo chake ni Wasambaza Habari wa France Le10sport.com, zimedai Kiungo huyo alishaafikiana maslahi yake binafsi na Man United na kilichobaki ni Klabu husika kukubaliana Ada ya Uhamisho.
Imedaiwa Man United imetoa Ofa ya Pauni Milioni 17 lakini Lazio wanataka Pauni Milioni 25 kwa Kiungo huyo mwenye Miaka 29.
Kuhusu Pedro, inasemekana Man United na Barcelona tayari wana makubaliano ila Barca wanataka Fowadi huyo abakie kwao hadi wamalize kucheza na Sevilla kwenye Fainali ya UEFA SUPER CUP itakayochezwa Jumanne huko Tbilisi, Georgia.
Klabu hizo mbili zimekubaliana Ada ya Uhamisho ya Pauni Milioni 18.1 ambayo itapanda kwa Pauni Milioni 4.2 kutokana na Bonasi mbalimbali za mafanikio ya Fowadi huyo.Ikiwa Pedro na Biglia watatua Old Trafford basi Wachezaji hao watafanya Man United iwe imepata Wapya 7 katika kipindi hiki kuelekea Msimu mpya kufuatia kusainiwa Memphis Depay, Matteo Darmian, Morgan Schneiderlin, Bastian Schweinsteiger na Sergio Romero.

0 maoni:

Post a Comment

waliotembelea blog