Friday, August 22, 2014

Na Baraka Mpenja
NUSU fainali ya klabu bingwa Afrika mashariki na kati, kombe la Kagame inaanza kutimua vumbi leo mjini Kigali, Rwanda.
Timu mbili pinzani za nchini Rwanda, Polisi na APR zitachuana vikali ili kupata timu moja ya kucheza fainali.
Polisi walifuzu hatua hiyo kufuatia kuwatoa Atletico ya Burundi hatua ya robo fainali kwa penati 9-8.
Mikwaju ya penalti ilitumika kuamua mshindi katika mechi hiyo kwasababu dakika 90 zilimalizika kwa suluhu pacha ya bila kufungana.
Kwa upande wa APR, wao walifanikiwa kufuzu nusu fainali kufuatia kuwachapa wapinzani wao Rayon Sport kwa penati 4-3.
Penalti ziliamua mshindi katika mechi hiyo kwa vile dakika 90 zilimalizika kwa sare ya mabao 2-2.
Mechi hii imevuta hisi za mashabiki wengi nchini Rwanda kutokana na timu hizo kucheza ligi moja, hivyo zinajuana vizuri kwa ubora na udhaifu wao.
Mbali na mchezo huo, nusu fainali nyingine itawakutanisha KCC ya Uganda dhidi ya El Merreik ya Sudan katika uwanja wa Nyamirambo, Kigali.

KCC walifuzu kwa kuifunga Altabara ya Sudan kusini katika mchezo wa robo fainali, wakati El Merreik waliifunga Azam fc ya Tanzania.

0 maoni:

Post a Comment

waliotembelea blog