Wednesday, September 11, 2013


ll
Mwanadada anayefanya vizuri sana kwenye muziki na filamu,baby Madaha amelamba bingo ya uhakika na kampuni ya Candy n’ Candy Records Label ya jijini Nairobi iliyomsainisha mkataba msanii mwingine wa Tanzania Mr.Nice hivi karibuni.
Akizungumza kwa simu na bongomovies leo meneja wa msanii huyo  Joe Kariuki amesema kuwa  pamoja na msanii huyo kupewa mkataba huo wa million hamsini (50) pia wamempa mwanadada huyo gari ya kutembelea ya kisasa aina ya AUDI TT na nyumba  kali mitaa kijitonyama jijini  Dar es salaam.
Pamoja na hayo pedeshee huyo wa Mr.Nice ambaye ndio mmiliki wa studio hiyo amesema wanataka kumuhamishia msanii huyo jijini Nairobi nchini Kenya kwa kipindi cha mwaka mmoja ili afanye nao kazi huko kwani wamegundua kuwa anakubalika sana nchini humo na wapenzi wa muziki.
Baby madaha ambaye  anatarajia kutua nchini leo akitoka Nairobi pamoja na meneja wake kwa ajili ya kuachia video ya  wimbo wake wa kwanza aliofanya na Label hiyo uitwao (Summer Holiday) ambao umefanywa huko huko jijini Naironi

0 maoni:

Post a Comment

waliotembelea blog