Mtaalamu: Ryan Giggs alifunga bao pekee la kufutia machozi katika kichapo cha mabao 5-1.
Kiungo mwalimu: Paul Scholes akimiliki mpira kuonesha kuwa ujuzi hauzeeki.
Winga mchawi: Kocha mpya msaidizi wa Manchester United, Ryan Giggs akimpiga chenga mpinzani wake wa Salford City
Majukumu ya ukocha: Nyota wa zamani wa Manchester United, Rio Ferdinand
MAGWIJI wa Manchester United wale wa kikosi cha
mwaka 1992 ‘Class of 92’ walishindiliwa kipigo kizito cha mabao 5-1 dhidi ya
timu ya daraja la chini ya Salford City jana usiku.
Salford ni timu ambayo inamilikiwa na magwiji,
Paul Scholes, Nicky Butty na Gary na Phil Neville.
Mchezo huo ulikuwa wa hisani na ulitazamwa na
mashabiki wapatao 12,00 katika dimba la
Aj Bell Mjini Eccles.
Katika mchezo huo, Mkongwe Ryan Giggs ambaye kwa sasa
ni kocha msaidizi wa Manchester United alimtamanisha kocha wake mkuu Louis Van
Gaal kwa kufunga bao moja la kufutia machozi katika kipigo hicho cha mbwa
mwizi.
Pamoja na kuzidiwa kasi na vijana wa timu hiyo
kutokana na umri kuwa mkubwa, lakini nyota hao wa zamani wa Man United
walionesha kiwango kizuri na kudhihirisha kuwa ujuzi hauzeeki.
Rio Ferdinand aliyesafiri kuwafundisha magwiji hao
kama kocha msaidizi, alishindwa kuwanusuru na kichapo.
0 maoni:
Post a Comment