Bingwa: James Wilson akiwa amebeba kombe la 'Manchester Senior Cup' baada ya kuingoza United kushinda mabao 4-1 dhidi ya Cit.
KINDA
wa Manchester United,James Wilson amemkumbusha Louis van Gaal umuhimu
wake kwa kufunga mabao yote manne katika ushindi wa 4-1 dhidi ya
mahasimu wao wakubwa Manchester City.
Timu hizo mbili hasimu zilikutana jana usiku katika mchezo wa fainali wa kombe la 'Manchester Senior Cup'.
Wilson
alifunga mabao mawili katika mechi yake ya kwanza ya ligi kuu dhidi ya
Hull City msimu uliopita chini ya kocha wa muda Ryan Giggs, lakini
hakuchukuliwa na Van Gaal katika ziara ya hivi karibuni ya maandalizi ya
msimu nchini Marekani.
Lakini
katika mechi ya jana iliyotazamwa na Manuel Pellegrini, Wilson
alionesha kiwango kikubwa na kubeba kombe hilo la 'Senior Cup' baada ya
kufunga mabao mawili katika kila kipinidi na kuifanya United ishinde
ikitokea nyuma.
Vipaji vya hali ya juu: James Wilson
alikuwa shujaa wa United, akifunga mara nne baada ya Man City
kutangulia kupata bao la kuongoza.
Katika mechi hiyo vijana walipeana changamoto kubwa na kuonesha jinsi gani wamebarikiwa kucheza soka.
Mwanzo mzuri: Jordi Hiwula, katikati kulia, akimpanda Devante Cole, kulia, baada ya kuifungia Man City bao la kuongoza
Kikosi cha Manchester City:
Gunn, Bossaerts, Maffeo, Bryan (Smith-Brown 46), Angelino, Glendon,
Ntcham (Horsfield 53), Fofana, Cole, Pozo (Ambrose 68), Hiwula
Wachezaji: O'Brien, Bytyqi.
Mfungaji wa goli: Hiwula.
Kikosi cha Manchester United: J Pereira; Vermijl, McNair, Thorpe, Varela; Janko, Pearson, Rothwell, Lawrence; A Pereira; Wilson
Wachezaji wa akiba: O'Hara, Harrop, Goss, Willock, Evans
Mfunagi wa magoli: Wilson (4).
Watazamaji: 3,261.
0 maoni:
Post a Comment