Wamekubaliana: Barcelona wameonekana kuwapiku Manchester United katika kumsajili, Thomas Vermaelen.
BARCELONA imekubali kulipa ada ya uhamisho ya paundi milioni 15 ili kuinasa saini ya beki wa Asernal, Thomas Vermaelen, na taarifa hizi ni pigo kubwa kwa mashetani wekundu, Manchester United waliotaka kumsajili.
Kilichobaki sasa ni makubaliani binafsi kati ya wakala wa Vermaelen na wakatalunya hao kabla ya kukamilika kwa dili hilo.
Jana jumatano, Barcelona walimtuma Raul Sanllehi kufanya makubaliano mjini London na wamefikia sehemu nzuri.
Wakatalunya wametoa ofa ya miaka mitano, huku kukiwepo kipengele cha kuongezewa mwaka mmoja zaidi na mshahara wa beki huyo utakuwa paundi elfu themanini.
Mazingira mapya? Barcelona wanaonekana kuelekea kumsajili Vermaelen kwa mkataba wa miaka minne na mshahara wa paundi elfu 80.
Hakuna kwenda: Arsenal walitaka kumuuza Vermaelen Man United kwa kubadilishana na Chris Smalling.
0 maoni:
Post a Comment