Na Baraka Mpenja
MICHUANO ya Kombe la Kagame inaanza kutimua vumbi
leo hii Agost 8 hadi 24 mwaka huu mjini Kigali nchini Rwanda, ambapo timu 14 zitawania taji linaloshikiliwa
na mabingwa watetezi, Vital’O ya Burundi.
Wawakilishi wawili wa Tanzania katika michuano
hiyo, KMKM ya visiwani Zanzibar na mabingwa Tanzania wa ligi kuu soka Tanzania bara,
Azam fc watashuka dimbani leo katika mechi za ufunguzi.
KMKM watacheza mechi ya ufunguzi ya kundi A dhidi
Altabara ya Sudan kusini katika uwanja wa Nyamirambo.
Wana Lambalamba, Azam fc waliopo kundi moja A timu hiyo ya Zanzibar, watajitupa uwanjani
jioni kuoneshana ufundi na wenyeji Rayon Sport katika dimba la taifa, Amahoro
mjini Kigali.
Azam fc waliokwenda Kigali na kikosi kamili gado
wanatazamiwa kutoa upinzani mkubwa wa Rayon ambao watakuwa na faida kubwa ya
mashabiki.
Baada ya mechi ya Azam, usiku katika dimba hilo
hilo, mchezo mmoja wa kundi B utachezwa baina ya timu ya zamani ya kocha wa
Simba sc, Zdrvako Logarusic na KCCA ya Uganda.
Kesho Agosti 9 mwaka huu katika dimba la
Amahoro mechi mbili za kundi C na moja
ya kundi B zitapigwa.
Mapema itaanza mechi ya mabingwa Vital’O ya
Burundi dhidi ya Benadir ya Somalia ikifuatiwa na mechi ya jioni baina ya
Police ya Rwanda na El Merreikh ya Sudan.
Baadaye usiku maafande wa jeshi, APR ya Rwanda watachuana
na Flambeau ya Burundi.
Azam fc watashuka dimbani tena Agosti 10 mchana
kuchuana na KMKM ya Zanzibar, mchezo wa kundi A.
0 maoni:
Post a Comment