BAADA ya kutolewa kushiriki michuano ya klabu bingwa
Afrika mashariki na kati maarufu kwa jina la kombe la Kagame, Yanga sc imesema
maisha mengine yanatakiwa kuendelea kama kawaida.
Katibu mkuu wa Yanga, Beno Njovu alisema
wamesikitishwa kutolewa Kombe la Kagame, lakini hali hiyo haiwafanyi washindwe
kuendelea na mipango mingine ya kuiandaa timu kwa ajili ya michuano iliyopo
mbele yao.
Njovu
alisema wachezaji waliotakiwa kwenda Kagame wanaendelea na mazoezi kama kawaida
na wale waliokuwa timu za taifa za nchi mbalimbali (Tanzani, Rwanda na Uganda) walipewa
mapumziko na wataripoti kesho jumamosi kwenye mazoezi ya timu yanayoendelea
uwanja wa shule ya sekondari Loyola,
Mabibo, jijini Dar es salaam.
“Maisha yanatakiwa kuendelea kama kawaida. Wale
wachezaji waliotakiwa kwenda Kagame, mnaona wanaendelea na mazoezi kama kawaida
na wale waliokuwa timu ya taifa wamepewa mapumziko mpaka jumamosi.” Alisema Njovu.
“Jumamosi wachezaji watafanya mazoezi. Wachezaji
wote waliokuwa na timu za taifa watakuwepo, halafu watakuwa na kikao na mwalimu
kupanga mikakati ya michuano iliyopo mbele yetu”
“Michuano iliyopo mbele yetu ilikuwa Kagame, lakini
kwasababu tumetolewa, sasa michuano iliyopo mbele yetu ni ligi kuu, wataanza
kupanga mikakati mara moja na kuingia kambini”
Baraza la vyama vya soka ukanda wa Afrika
mashariki na kati CECAFA iliwatoa Yanga kushiriki kombe la Kagame baada ya kukataa
kutuma kikosi cha kwanza.
Awali Yanga ilituma kikosi cha pili cha wachezaji
20, lakini CECAFA ikakitaa na kuitaka klabu hiyo kuthibitisha kutuma kikosi cha
kwanza, lakini wanajangwani hawakufanya hivyo na wakatupwa nje ya michuano.
Baada ya tukio hilo, CECAFA waliwasiliana na TFF
na kulitaka Shikirikisho hilo kuchagua timu nyingine na zali likawaangua Azam
fc.
0 maoni:
Post a Comment