Mpya: Msimu ujao Ligi kuu nchini England imethibitisha matumizi ya dawa hii ya kupulizia.
BAADA ya kuthibitisha matumizi ya dawa
maalumu ya kupulizia, ile inayokauka haraka na alitumiwa kombe la dunia,
bodi ya ligi kuu England imeripotiwa kuagiza chupa 2,000 kwa ajili ya
marefa msimu ujao, kwa mujibu wa gazeti za Daily Telegraph.
Waamuzi watamaliza msimu ujao wakiwa na
dawa hiyo ambayo itawasaidia kuweka alama umbali wa mita 10 kutoka
kwenye mpira pale inapotokea adhabu ndogo na mabeki wanatakiwa kuweka
ukuta.
Mkurugenzi mkuu wa ligi kuu, Richard
Scudamore alisema: 'Tunaenda sambamba na maendeleo yanayoongeza
ushindani na tulitazama kombe la dunia na kuona dawa ya kupuliza
iliyotumika na waamuzi, hakika iliwasiaida marefa, wachezaji na wale
wote waliokuwa wanaangalia mechi".
0 maoni:
Post a Comment