Saturday, March 14, 2015


sylvestermarshAliyekuwa Kocha msaidizi wa zamani wa Timu ya Taifa ya Tanzania, Sylvester Marsh amefariki dunia leo asubuhi katika hospitali ya Taifa ya Muhimbili.
Kocha huyo (Marsh) alikuwa akisumbuliwa na ugonjwa wa kansa ya koo na hivi karibuni alisafirishwa kutoka Mwanza hadi jijini Dar es Salaam.
Hata hivyo, hali ya Marsh pia aliyewahi kuwa Kocha Msaidizi wa Kilimanjaro Stars pia alizinoa timu kadhaa za Ligi Kuu Bara iliendelea kuwa mbaya kadiri siku zinavyosonga mbele.
Pamoja na hivyo suala la afya yake liliendelea kuwa siri kubwa huku baadhi ya wadau wakisumbuka kutafuta wodi aliyolazwa.
Aliwahi kuugua taabani na kukawa na taarifa za Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) kumtelekeza. Lakini baadaye lilikanusha.
Mdau, Abdulfatah Saleh ambaye ni mmiliki wa Hoteli ya Sapphire Court ya Kariakoo jijini Dar es Salaam ndiye alijitolea kumhudumia katika matibabu yake.
Ingawa alikuwa hapendi watu wajue, lakini mdau huyo ndiye alifanya kila, juhudi kuhakikisha Marsh anapata matibabu bora hadi alipopata nafuu na kurejea kwao Mwanza.

0 maoni:

Post a Comment

waliotembelea blog