Saturday, March 14, 2015


Manuel Pellegrini ana hakika hatafukuzwa kazi mwishoni mwa Msimu.
Bosi huyo wa Manchester City yupo kwenye presha kubwa ya kuleta mafanikio na hasa Timu yake kutetea Taji lao la Ubingwa wa Ligi Kuu England.
Hadi sasa, Man City wameshatupwa nje ya Makombe mawili ya England, FA CUP na CAPITAL ONE CUP, na huko Ulaya kwenye UEFA CHAMPIONS LIGI wapo mguu nje baada ya kuchapwa 2-1 na FC Barcelona wakiwa kwao Etihad na watarudiana huko Nou Camp Wiki ijayo.
Huku kukiwa na tetesi Mtaliana Carlo Ancelotti, Bosi wa Mabingwa wa Ulaya Real Madrid, yuko mbioni kutua Etihad Msimu ujao, Pellegrini amesisitiza Mkataba wake ni hadi Juni 2016.
Jumamosi, City wako Ugenini kucheza Mechi ya Ligi Kuu England na Burnley huku wao wakiwa Nafasi ya Pili Pointi 5 nyuma ya Vinara Chelsea ambao wamecheza Mechi 1 pungufu.
Mwishoni mwa Desemba, Uwanjani Etihad, Burnley walitoka nyuma 2-0 na kutoka Sare 2-2 na tangu wakati huo City wameshinda Mechi 3 tu za Ligi.
Mbali ya presha yake binafsi, Pellegrini pia amelazimika kukanusha tuhuma za Magazeti ya Uingereza kuwa amempiga Benchi Nahodha Vincent Kompany baada ya kudaiwa kugombana na Mchezaji mwenzake Fernandinho.
Straika wa Chelsea Diego Costa akimsonga Ibrahimovic na kumshinikiza refa Bjorn Kuipers kutoa kadi nyekundu

Wachezaji wa Chelsea wakimzunguka Mwamuzi Kuipers wakati wa mchezo wa Uefa Champions Ligi dhidi ya PSG kitendoambacho kocha wa City amekiponda kwamba Wachezaji wake hawawezi kufanya Uwanjani.

Ibrahimovic mpaka alipewa kadi Nyekundu katika Mtanange huo ambao Chelsea waliondoshwa licha ya Chelsea kucheza 11 Uwanjani na wenzao pungufu 10 PSG.

0 maoni:

Post a Comment

waliotembelea blog