Mbwana Samatta ni mshambuliaji wa kimataifa kutokea Tanzania anaeichezea klabu ya TP Mazembe ya Jamuhuri ya Kidemokrasia ya Congo ambayo alijiunga nayo mwaka 2011 akitokea Simba ya Tanzania na mpaka sasa amekua mmoja kati ya wachezaji mahiri wanaounda safu imara ya ushambuliaji kwa TP Mazembe na timu ya taifa ya Tanzania.
Samatta aliingia kwenye headlines siku kadhaa zilizopita baada ya kukataa kusajiliwa na klabu ya Zamalek ya Misri kwa euro milioni 1 kutoka TP Mazembe ambayo ni sawa na zaidi ya bilioni 2.3 za Kitanzania, kila media iliandika hii story nakuonekana kama Samatta amepoteza bahati.
Wakala wa mchezaji huyo Jamal Kasongo amezungumzia suala hilo na mpango wa Samatta licha ya kupewa ofa ya mshahara mkubwa.
“La
kwanza ni kweli maafisa wa Zamalek wawili walifika kipindi mimi nipo na
Mbwana kipindi yupo katika mechi ya timu ya taifa kimsingi mimi
niliweza kukaa nao chini kuweza kufanya nao majadiliano lakini lazima
mchezaji ili ufikie malengo uweze kukaa katika mstari, msimamo wa Mbwana
na msimamo wangu mimi kama mshauri wake ni Mbwana kuweza kucheza
Ulaya”>>>Jamal Kasongo
“Wakatuma
tena ofa wako tayari kumnunua TP Mazembe kwa euro milioni 1 na euro
milioni 1 ni pesa nyingi na walikuwa tayari wakimuhitaji waweze kumpa
mshahara ambao hakuna mchezaji ndani ya Afrika hii anaweza akalipwa
lakini bado hili suala lilikuwa gumu kwani lengo kubwa ni Mbwana kucheza
Ulaya”>>>Jamal Kasongo
0 maoni:
Post a Comment