Manchester
United wameshindwa kutetea Taji lao la International Champions Cup
baada ya kufungwa 2-0 na Paris Saint-Germain kwenye Mechi yao ya mwisho
Usiku wa kuamkia Leo huko Soldier Field, Chicago, USA na kuiacha PSG
ikibeba Kombe hilo.PSG
walifunga Bao lao la kwanza katika Dakika ya 25 baada Mpira mrefu
kutoka kwa Silva kumkuta Kipa David De Gea akiwa nafasi ovyo na Blaise
Matuidi kuutokea na kufunga.Dakika
9 baada PSG walifunga Bao la Pili kupitia kupitia Straika wao hatari
Zlatan Ibrahimovic aliepokea pasi kutoka kwa Lucas Moura na kumpa
Maxwell alietumbukiza Krosi ndani ya boksi na kuunganishwa wavuni na
Ibrahimovic.
Hadi Mapumziko PSG 2 Man United 0.Mechi
hii ilikuwa ni mechi ya 4 na ya mwisho kwa Man United wakiwa Ziarani
huko USA na walishinda mechi zao 3 za awali kwa kuziangusha Club America
ya Mexico (1-0), San Jose Earthquakes ya USA (3-1) na Barcelona (3-1).Katika mchezo huo kukaba ndio ilikuwa nguzo!!
Zlatan Ibra
Michael Carrick
Depay
Ndani ya Uwanja wa Soldier Field, Chicago, United States
Manchester United mpaka sasa hajapata bao, Paris Saint-Germain
wanaongoza bao 2-0 zilizofungwa kipindi cha kwanza dakika ya 25 na
Blaise Matuidi na lilie la dakika ya 34 na Zlatan Ibrahimovic.
0 maoni:
Post a Comment