Msanii maarufu wa Hip Hop Marekani Tyga ameingia kwenye headlines baada ya taarifa kusambaa kuwa msanii huyo yupo matatani kufukuzwa kwenye nyumba yake iliopo Calabasas kwa kukwepa kulipa kodi ya nyumba hiyo kwa miezi miwili.
Nyumba hiyo ni nyumba aliyokuwa akiishi na aliyekuwa girlfriend wake Blac Chyna na thamani ya kodi ya nyumba hiyo ni dola 25,ooo kwa mwezi sawa na Mil.50 za Kitanzania, deni lake la miezi 2 linagonga mpaka Mill.100!
Mwenyenyumba anasema hii sio mara ya kwana kwa msanii huyo wa Young Money kukwepa kulipa kodi ya nyumba hiyo, na amempa mpaka jumamosi ya wiki hii kukamilisha deni hilo.
Kama Tyga hatolipa kodi hiyo basi mwenyenyumba atalazimika kutoa notice ya kumuondoa kwenye nyumba hiyo na atamtoza msanii huyo dola 833 kwa siku mpaka atakapo ondoka ambayo ni sawa na Mil. 1,666,000 za Tz.
Mwezi wa 5 Tyga alishitakiwa kukwekpa kulipa kodi ya nyumba nyingine thamani yake ilikuwa karibia dola 125,000 na kwa sasa ana kesi Mahakamani ya dola Mil.1.6.
0 maoni:
Post a Comment