Thursday, July 30, 2015


Licha ya kuhuzunishwa kufungwa 2-0 na Paris Saint-Germain huko Soldier Field, Chicago, USA, Meneja wa Manchester United Louis van Gaal ameridhika na Timu yake na kudai kufungwa huko kutawasaidia.
Kipigo hicho kimeifanya Man United washindwe kutetea Taji la International Champions Cup licha ya kushinda Mechi 3 ikiwemo ile waliyowatwanga 3-1 Mabingwa wa Ulaya Barcelona.
Lakini Van Gaal amesema kufungwa kwao kunatokana na makosa binafsi walipofungwa Bao la kwanza kwa kujifunga mwenyewe Luke Shaw alipojichanganya na Kipa wake David de Gea.
Van Gaal amesema: "Ndio tumefungwa pengine hiyo ni viziri kwani Mwaka Jana tulishinda Mechi zote tukaja kufungwa Mechi ya Kwanza ya Ligi."

Mechi ijayo kwa Man United ni hapo Jumamosi Agosti 8 Uwanjani Old Trafford na Tottenham ikiwa ni Mechi yao ya kwanza ya Ligi Kuu England. 
Pia, Van Gaal amedokeza kuitumia Fomesheni ya 4-3-2-1 kwa kuwachezesha Mafulbeki Luke Shaw na Matteo Darmian huku Sentahafu akiwa Daley Blind akisaidiwa na Mtu mwingine ambae hakumtaja.
Ibrahimovic, who has admitted he would be happy to work with Louis van Gaal, started and finished the move for PSG's second goalKuhusu kuntumia Blind kama Sentahafu Meneja huyo amesema Mchezaji huyo huanzisha vyema mipira na pia mzuri katika kujihami.

0 maoni:

Post a Comment

waliotembelea blog