Thursday, July 30, 2015

Louis-Van-Gaal-Press-Conference
Wakati klabu ya Paris Saint Germain (PSG) ya Ufaransa ikizidi kusisitiza kuwa uhamisho wa mchezaji wa Manchester United Angel Di Maria kwa asilimia kubwa umekamilika, kocha wa Manchester United Louis van Gaal amezungumza kitu cha kushangaza kidogo kuhusiana na Di Maria.
Di-Maria
Di Maria alishindwa kuripoti July 25 San Jose kujiunga na timu na kuanza mazoezi ya maandalizi ya msimu mpya Ligi Kuu… Baada ya mchezo wa International Champions Cup kati ya Man Uninted dhidi ya PSG kumalizika kwa Man United kufungwa kwa goli 2-0, Van Gaal akiwa kwenye Press Conference alijibu hafahamu nyota huyo alipo.
angel-di-maria
“Sijui wapi alipo”>>>Van Gaal
Licha ya kocha wa PSG  Laurent Blanc kuthibitisha kuwa mazungumzo kuhusiana na uhamisho wa Di Maria yamekaribia kufikia ukingoni ingawa Man United inataka pound milioni 28 ili imuachie nyota huyo.
“Manchester United na Paris Saint Germain ni vilabu viwili vikubwa na makubaliano yanaweza kuwa magumu lakini tunakaribia kufikia muafaka”>>> Laurent Blanc
football-premier-league-angel-di-maria-manchester-united_3197494
Di Maria alihamia Manchester United mwaka 2014 akitokea katika klabu ya Real Madrid ya Hispania kwa dau la uhamisho pound milioni 59.7 kwa mkataba wa miaka mitano kiasi ambacho kilileweka rekodi ya uhamisho Uingereza.
1409352274270_wps_89_Manchester_United_new_sig

0 maoni:

Post a Comment

waliotembelea blog