Tuesday, October 20, 2015


KIKOSI cha Wachezaji 20 wa Manchester United Leo hii wamesafiri kwenda Moscow, Urusi ambako Kesho Usiku watacheza Mechi yao ya Kundi B la UEFA CHAMPIONS LIGI, UCL, na CSKA Moscow.Kikosi hicho kimeundwa na Wachezaji 18 ambao ndio walicheza na kuwa Benchi Jumamosi iliyopita huko Goodison Park walipoichapa Everton Bao 3-0 kwenye Mechi ya Ligi Kuu England.
Wachezaji Wawili walioongezwa ni Kipa Sergio Romero na Antonio Valencia.

Kwenye Kundi B kila Timu ina Pointi 3 baada ya Mechi 2 na Mechi hizi za 3 ni muhimu katika kufungua njia ya kufuzu kwenda Raundi ya Mtoano ya Timu 16.

Mechi nyingine kali za UCL ambazo zitachezwa Kesho ni ile ya Jijini Manchester Uwanjani Etihad wakati Man City wakiikaribisha Sevilla ya Spain kwenye Mechi ya Kundi D na huko Jijini Paris Nchini France ipo Mechi ya Kundi A kati ya Paris St Germain na Real Madrid.
MAN UNITED WACHEZAJI 20 WALIOKWEA NDEGE NI
De Gea, Romero, Johnstone, Darmian, Smalling, Jones, Rojo, Blind, Carrick, Schweinsteiger, Schneiderlin, Fellaini, Valencia, Pereira, Mata, Herrera, Memphis, Lingard, Rooney, Martial.

Meneja wa Man United Van Gaal

Wayne Rooney

UEFA CHAMPIONS LEAGUE
MAKUNDI
Jumanne Oktoba 20
KUNDI E

BATE Borislov v Barcelona
Bayer Leverkusen v AS Roma

KUNDI F

Arsenal v Bayern Munich
Dinamo Zagreb v Olympiakos

KUNDI G

Dynamo Kiev v Chelsea
FC Porto v Maccabi Tel Aviv

KUNDI H

Valencia v KAA Gent
Zenit Saint Petersburg v Lyon

0 maoni:

Post a Comment

waliotembelea blog