Saturday, June 14, 2014


Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta ameizawadi kwa kuifadhili timu ya taifa ya soka Harambe Stars ziara ya kwenda Brazil kutazama michuano ya kombe la dunia Hafla ya kuikabidhi rasmi ufadhili huo timu hiyo, ilifanyika katika ikulu ya Rais Ijumaa ambapo wachezaji kumi na moja wa timu hiyo walikabidhiwa tiketi za ndege kwenda Brazil. Kitendo cha Rais bila shaka ni jambo la kutaka kuwatia motisha wachezaji wa timu ya taifa ambao hivi karibuni waliicharaza Djibouti mabao mawili kwa moja katika duru ya kwanza ya michuano ya kuwania kombe la taifa bingwa Afrika baadaye mwakani.Rais Kenyatta akiongea na Wachezaji wa Timu hiyo.
Hapa Akigawa tiketi huku akishuhudiwa na mkewe Bi. Margaret Kenyatta na seneta wa Nairobi Mike Sonko (kushoto).
Picha ya Pamoja.

0 maoni:

Post a Comment

waliotembelea blog