Monday, March 17, 2014


Steven Gerard alifunga mikwaju miwili ya penalty na kukosa ya tatu Liverpool ikiendelea kuimarisha matokeo yake baada ya kuwacharaza mabingwa watetezi wa ligi ya uingereza Machester United tatu bila katika uga wao wa nyumbani Old Trafford.
Katika kile kilichoonekana kama harakati za kushinda taji lao la kwanza tangia mwaka 1990,Liverpool ilipita mtihani wao kwa kuonyesha mchezo mzuri dhidi ya timu ya Manchester United ambayo haikuweza kuwadhibiti wapinzani wao na hivyobasi kusogea hadi nafasi ya pili na pointi nne nyuma ya viongozi wa ligi hiyo Chelsea.
Nahodha wa Liverpool Gerard alionyesha uongozi wake huku wakifazawadiwa mikwaju ya penalty katika vipindi vyote viwili huku timu hiyo ya meneja Brenda Rodgers ikitawala dhidi ya timu ya Machester ambayo inahitaji marekebisho makubwa.
Kutokana na mechi hizo za leo Chelsea iko katika nafasi nzuri ya kushinda taji hilo kwa alama 66 ikiwa imecheza mechi 30 huku timu za liverpool na Arsenal zikiwa na pointi 62 kila mmoja, lakini liverpool inashikilia nafasi ya pili kwa wingi wa mabao.
Arsenal ni ya tatu huku Manchester City iliocheza mechi 27 ikiwa na pointi 60 na hivyobasi ikifunga udhia wa time nne bora

Wachezaji wa Liverpool wakipongezana baada ya kuwafunga United Old TraffordLiverpool leo imejichukulia pointi tatu baada ya kuwalaza Manchester United kwenye Uwanja wao Old Trafford. Liverpool wameanza kupata kupita mchezaji wake Kapteni Steven Gerrard kwa mkwaju wa penati katika dakika ya 34 kipindi cha kwanza, Baada ya Rafael kuunawa mpira kwenye eneo hatari la penati. Liverpool 1-0 dhidi ya wenyeji United. Mapumziko Liverpool inaongoza bao 1-0.
Kipindi cha pili Dakika ya 46 Liverpool wanapata penati nyingine, Ni baada ya Jones kumfanyia rafu kwa kumwangusha Allen chini. Steven Gerrard anawapachika bao kwa mkwaju huo na kufanya bao 2-0 dhidi ya Manchester United kwenye uwanja wa Old Trafford.
Dakika ya 77 Nemanja Vidic aliondoshwa nje kwa kadi nyekundu baada ya kufanya rafu kwa Sturridge na mwamuzi kumtoa kwa kadi hiyo nyekundu huku Vidic akimlalamikia kwamba kajiangusha na
Dakika ya 78 Steven Gerrard alikosa penati hiyo iliyogonga mwamba na kurudi ndani na mchezaji wa Man United kuuondosha.
Dakika ya 84 Luis Suárez alipachikia bao la tatu Liverpool na kufanya 3-0 dhidi ya United baada ya mabeki wa United kupitiwa wakidhani ni faulu.
Ushindi huu wa Majogoo Liverpool unawapandisha hadi nafasi ya pili wakiwa na pointi 62, Nyuma ya pointi 4 ya vinara Chelsea wenye pointi 66 waliofungwa jana na Aston Villa.Steven Gerrard (kushoto) akishangilia bao lake 






Van Persie chupu chupu atupie bao hapa!!



0 maoni:

Post a Comment

waliotembelea blog