Tuesday, July 22, 2014


Kuanzia kushoto, Luis Figo, Zinedine Zidane na Ronaldo de Lima

Na Baraka  Mpenja, Dar es salaam

Imechapishwa Julai 22, 2014, saa 11:26 jioni

VODACOMA Tanzania ni miongoni mwa makampuni yaliyojitokeza kudhamini ziara ya magwiji waliocheza kwa mafanikio makubwa katika klabu ya Real Madrid.
Kikosi cha magwiji hao maarufu kama `Real Madrid Legends` kitafanya ziara ya siku nne nchini kuanzia Agosti 22 mwaka huu na kitacheza mechi moja ya kirafiki dhidi ya kikosi maalumu cha nyota wa Tanzania.
Akizungumza leo na waandishi wa habari katika hoteli ya New Afrika, jijini Dar es salaam, meneja wa ziara hiyo, Dennis Ssebo amesema  mbali na Vodacom, wadhamini wengine ni Fastjet, Tropical, Pembe Flower, Lake Gas, EFM Radio na Ladger Plaza Bahari Beach.
Ziara hiyo ni mwaliko wa kampuni ya Tanzania Sisi ni Nyumbani (TSN), chini ya mkurugenzi wake mkuu, Farough Baghozah na meneja wa ziara hiyo ni Dennis Ssebo.
Wachezaji wa Real Madrid waliocheza La Liga miaka ya nyuma, ligi ya mabingwa kombe la dunia kama vile Mfaransa Zinedine Zidane, Mreno Luis Madeila Figo na Mbrazil Ronaldo de Lima watakuwepo katika ziara hiyo.
Ssebo kabla ya mkutano wa leo, aliuambia mtandao huu kuwa maandalizi ya ziara hiyo yanakwenda vizuri na itakuwa fursa pekee kwa Watanzania kuiona Real Madrid kwa mara ya kwanza barani Afrika.
 “Ninaloweza Kusema ni kwamba,  Watanzania wakae tayari kupokea wachezaji 27 wa zamani wa timu ya Real Madrid na mashabiki 23  kutoka Hispania wanaokuja kuwashangilia magwiji wao. Kwahiyo jumla tunapokea watu 50 kutoka Hispania kwa ajili ya ziara hii”. Alisema Ssebo.

“Ni ziara ambayo tulifikiria itakuwa fupi, lakini wenzetu kumbe wameipenda nchi na wanaifahamu, kwahiyo ni ziara ambayo itachukua takribani siku nne”. Aliongeza.

0 maoni:

Post a Comment

waliotembelea blog