RASMI Real Madrid wamekamilisha kumsajili mfungaji bora wa kombe la dunia, James Rodriguez kutoka klabu ya Monaco.
Nyota huyo wa kimataifa wa Colombia
amekubali kusaini mkataba wa miaka sita na alichukuliwa vipimo vya afya
leo asubuhi na atatambulishwa jioni hii.
Hakuna klabu yoyote iliyothibitisha ada
ya uhamisho ya mchezaji huyo mwenye miaka 23, lakini ripoti zinasema
Madrid wamelipa paundi milioni 60 zitakazomuweka Rodrigues kuwa mchezaji
namba nne katika orodha ya wachezaji ghali zaidi duniani.
Mchezaji ghali zaidi duniani ni Gareth Bale, akifuatiwa na Cristiano Ronaldo na Luis Suarez.
Dili limekamilika: James Rodriguez alipimwa afya leo asubuhi.
Hapa dole sasa!: Rodriguez anakuwa mcheza namba nne katika orodha ya wachezaji ghali zaidi duniani
Tayari: Rodriguez akiondoka katika hospitali ya le Sanitas La Moraleja baada ya kupima afya mjini Madrid.
0 maoni:
Post a Comment