Tuesday, July 22, 2014


Straika wa Manchester City, Mabingwa wa England, Alvaro Negredo, amevunjika Mfupa mdogo wa Mguuni na kufuta matumaini ya yeye kurudi kwao Spain kucheza Klabu ya huko.
Negredo, mwenye Miaka 28, aliumia Siku ya Ijumaa wakati City wanajipima na Hearts huko Scotalnd na kushinda Mechi hiyo 2-1.
Taarifa za awali zimedai atakuwa nje ya Uwanja kwa Miezi kadhaa.
Msimu uliopita Negredo aliifungia City Bao 23 katika Mechi 33 alizocheza lakini kwenye Mechi 16 alizocheza mwisho hakufunga hata Bao.

USAJILI ENGLAND: MATS HUMMELS KUJIUNGA NA KLABU YA MANCHESTER UNITED

Sentahafu wa Germany na Klabu ya Borussia Dortmund Mats Hummels kujiunga na Manchester United kabla Wikiendi hii kufika.
Hivi sasa Klabu hizo mbili zipo kwenye mazungumzo mazito lakini habari zilizovuja zimedai makubaliano yatafikiwa hivi karibuni.
Confident: Van Gaal is looking to build a squad capable of challenging at the very top
Hummels, mwenye Miaka 25, aling’ara huko Brazil wakati Germany ilipotwaa Kombe la Dunia kwa kuichapa Argentina Bao 1-0 kwenye Fainali iliyochezwa Julai 13 huko Maracana, Rio de Janeiro.
Ikiwa Uhamisho huu utakamilika, Hummels atakuwa Mchezaji wa 3 kununuliwa na Meneja mpya Louis van Gaal, baada ya Ander Herrera na Luke Shaw, lakini umuhimu wake ni mkubwa sana kwani Man United imeshapoteza Mabeki wazoefu watatu walioondoka, ambao ni Nemanja Vidic, Rio Ferdinand na Patrice Evra, na kuja kwake kutaimarisha safu ya ulinzi.
Crucial: Hummels will be sorely missed at Dortmund if he leaves
Pia, kuja kwa Mjerumani huyo kutawapa moyo sana Mashabiki wa Man United baada ya Jana Makamu Mwenyekiti Mtendaji wa Klabu hiyo, Ed Woodward, kusema wategemee Wachezaji wapya katika Wiki chache zijazo.

Woodward alitamka: “Hamna kiwango cha Bajeti kilichowekwa. Kifedha tuna nguvu sana, zipo Fedha za Uhamisho. Louis ndie Bosi na anatathmini nini kinaendelea lakini tumekuwa na mazungumzo na walengwa na kazi inaendelea nyuma ya pazia. Tunasonga mbele kwa baadhi ya walengwa hao…hivyo kaeni chonjo hapa!”

Aliongeza: “Louis anapata muda zaidi wa kufanya tathmini yake na ikibidi tutabadilisha maamuzi na kufanya mengine. Tunataka kuchukua hatua thabiti ili kutwaa Ubingwa!”

0 maoni:

Post a Comment

waliotembelea blog