Tuesday, July 22, 2014


Patrce Evra anaondoka Manchester United na kuhamia Juventus baada ya kudumu Miaka 8 na Nusu Old Trafford kwa mujibu wa habari zilizothibitishwa na Klabu zote mbili.
Evra anaondoka Man United mara tu baada ya Meneja mpya Louis van Gaal kumsaini Kijana wa Miaka 19 Luke Shaw kutoka Southampton kuziba pengo lake.
Juventus imempa Evra Mkataba hadi 2016 na watailipa Man United Euro Milioni 1.2 kwa mikupuo miwili na Euro Laki 3 zaidi ikiwa Msimu ujao watafuzu kucheza UEFA CHAMPIONS LIGI.
Evra alitoa ujumbe kwa Mashabiki wa Man United na kuwaambia: “Baada ya kufikiri sana nimeamua sasa ni muda muafaka kuondoka Manchester United. Ni uamuzi mkubwa mno katika maisha yangu ya Soka kwa sababu Klabu hii, na Siku zote itabaki hvyo, ipo moyoni mwangu!”
Akiwa na Man United, Evra alicheza Mechi 379 na kufunga Bao 10 katika Misimu 9.
Evra, anaetoka France, alijiunga na Man United Januari 2006 kutoka Monaco ambako, akiwa na Miaka 24 tu, alikuwa Nahodha wao na kucheza Fainali ya UEFA CHAMPIONS LIGI Mwaka 2004.
Mwanzoni Evra alikuwa na wakati mgumu akiichezea Man United na katika Mechi yake ya kwanza kabisa dhidi ya Man City waliyofungwa 3-1, alitolewa wakati wa Haftaimu.
Lakini baada ya Miezi 6 tu alimpora namba Gabriel Heinze na kuisaidia Man United kutwaa Ubingwa Msimu wa 2006/07.
Akiwa na Man United, Evra alitwaa Ubingwa wa England mara 5, Ligi Cup 3, UEFA CHAMPIONS LIGI na Klabu Bingwa ya Dunia.
Pia amewahi kuteuliwa kwenye Timu ya Mwaka ya PFA [Chama cha Wachezaji Soka wa Kulipwa] mara 3, kwenye Misimu ya 2006/07, 2008/09, 2009/10, na Mwaka 2009 alikuwemo kwenye Kikosi cha Mwaka cha UEFA na kile Kikosi cha Dunia cha FIFA FIFPro.
Wakati Nemanja Vidic alipokuwa majeruhi, Evra ndie alikuwa akikaimu Nafasi ya Nahodha wa Mnchester United.

0 maoni:

Post a Comment

waliotembelea blog