Na Baraka Mpenja, Dar es salaam
KUMEKUCHA! Ndivyo unaweza kusema!.
Baraza la vyama vya soka kwa ukanda wa Afrika mashariki na kati, CECAFA limetoa
ratiba ya michuano ya klabu bingwa Afrika mashariki na kati,maarufu kwa jina la
`Kagame Cup` itakayofanyika mwaka huu, mjini Kigali nchini Rwanda kuanzia Agost
8.
Mabingwa wa Tanzania msimu wa
2012/2013, Dar Young Africans wataanza kampeni ya kusaka taji hilo Agosti 8
mwaka huu dhidi ya Rayon katika dimba la
Amahoro mjini Kigali.
Hii itakuwa mechi ya kwanza ya
mashindano kwa kocha mkuu wa Wanajangwani, Mbrazil Marcio Maximo aliyetua Yanga
mwaka huu baada ya Mholanzi Hans van Pluijm kumaliza mkataba wake na kutimkia
Saudi Arabia sambamba na aliyekuwa msaidizi wake Charles Boniface Mkwasa
`Master`.
Andrey Coutinho (kushoto) akipasha moto misuli
Pia wachezaji wawili raia wa Brazil, Gleison Santos Santana na Andrey Coutinho watacheza mechi yao ya kwanza siku hiyo wakiwa kwenye uzi wa njano au kijani.
Andrey Coutinho (kushoto) akipasha moto misuli
Pia wachezaji wawili raia wa Brazil, Gleison Santos Santana na Andrey Coutinho watacheza mechi yao ya kwanza siku hiyo wakiwa kwenye uzi wa njano au kijani.
Mechi nyingine siku ya ufunguzi
itawakutanisha Atlabara
dhidi ya KMKM ya Zanzibar kwenye uwanja wa Nyamirambo, wakati Gor Mahia ya
Kenya itacheza dhidi ya KCCA.
Agosti
10 mwaka huu, Yanga watacheza mechi ya pili ya kundi A dhidi ya Watanzania
wenzao, KMKM ya Zanzibar. Na Agosti 12 mwaka huu Maximo ataiongoza tena Yanga kupepetana
na Atlabara.
Agosti
16 Yanga itaoneshana kazi na Coffee katika mchezo wa mwisho wa kundi A.
Robo
fainali ya kombe la Kagame itaanza kutimua vumbi Agosti 19 mwaka huu.
Afisa
habari wa CECAFA , Rogers Mulindwa katika taarifa yake mchana huu amesema muda
wa kuanza kwa mechi utapangwa kwa makubaliano kati ya CECAFA, shirikisho la
soka nchini Rwanda (FERWAFA) na kituo cha luninga cha Supersport ambacho kitarusha
moja kwa moja michuano hiyo.
Michuano
ya Kagame ndio sababu kubwa ya shirikisho la soka Tanzania TFF, kusogeza mbele michuano ya ligi kuu soka
Tanzania bara hadi septemba 20 mwaka huu kwa lengo la kuwasubiri Yanga.
Awali
ligi kuu ilitakiwa kuanza kushika kasi Agosti 24 mwaka huu, lakini kutokana na
sababu tofauti kubwa ikiwa ni hiyo ya Kagame, ratiba akapigwa teke.
Yanga
kwasasa wanaendelea na mazoezi ya kujiweka fiti kuelekea katika michuano hiyo
katika uwanja wa shule ya Sekondari Loyola.
Kocha
Maximo alisema ataitumia michuano ya Kagame kuona kikosi chake ili kujua mapungufu
yako wapi na kuyarekebisha kabla ya kuanza ligi kuu.
Hata
hivyo wachezaji wa Yanga waliopo katika kikosi cha timu ya Taifa ya Tanzania
kinachojiandaa na mechi ya marudiano dhidi ya Msumbuji wiki mbili zijazo, hawapo
kwenye Mazoezi hayo.
Wachezaji
walipo Taifa stars ni Deogratius Munish `Dida`, Oscar Joshua, Kelvin Yondani,
Nadir Haroub `Cannavaro`, Saimon Msuva na Mrisho Khalfani Ngassa.
Pia
nyota wake wa kimataifa, Emmanuel Okwi, Khamis Kiiza `Diego` (Uganda) na Haruna
Niyonzima (Rwanda) wapo katika majukumu
ya timu zao za taifa katika michuano ya mtoana kusaka tiketi ya kucheza michuano
ya kombe la shirikisho barani Afrika, AFCON mwakani nchini Morroco.
0 maoni:
Post a Comment