Matajiri wapya katika soko la usajili barani ulaya klabu ya AS Monaco imesema kwamba walipewa ofa ya kumnunua winga wa klabu ya Manchester United Nani.
Winga huyo wa timu ya taifa ya Ureno amekuwa njia panda kujua hatma yake ndani ya Old Trafford kabla ya kustaafu kwa Sir Alex Ferguson mpaka sasa chini ya manager mpya David Moyes.
Billionea anayemiliki klabu ya Monaco - Vadim Vasilyev amekiri kwamba United walimpa ofa ya kumsajili Nani.
Alisema: “Nani tulipewa ofa kumnunua. Ni mchezaji mzuri, lakini hakujawahi kuwa na mazungumo mpaka sasa.”
Monaco wamekuwa na vurugu sana kwenye soko la usajili hivi karibuni, wakiwasajili wachezaji kama Falcao, James Rodriguez Joao Moutinho kwa bei mbaya sana.

0 maoni:
Post a Comment