Friday, August 21, 2015


Ikiwa imebakia siku moja kabla ya mchezo unaosubiri kwa hamu na mashabiki wa soka Tanzania kuuona, mchezo wa ngao ya Hisani kati ya Yanga na Azam FC, klabu ya Azam FC imethibitisha kuwakosa nyota wake kadhaa akiwemo Allan Wanga aliyekwenda Kenya wiki moja iliyopita kwa ajili ya msiba wa mama yake.
pacha
Lakini pia itamkosa mshambuliaji kutoka Ivory Coast Kipre Bolou ambaye pia ni majeruhi lakini taarifa zilizotoka siku ya Ijumaa August 21 ni kuwa klabu ya Azam FC imeamua kumpeleka nyota huo Afrika Kusini kwa ajili ya matibabu zaidi, kupitia afisa habari wa klabu hiyo Jaffar Iddi Maganga, Bolou atakaa Afrika Kusini kwa wiki mbili.
6Ikumbukwe kuwa Kipre Bolou ni ndugu wa damu na Kipre Tchetche ambao wote wanaitumikia klabu ya Azam FC ambayo ni makamu bingwa wa msimu uliopita na alikuwa bingwa wa msimu uliomalizika.

0 maoni:

Post a Comment

waliotembelea blog