Tuesday, April 22, 2014


UEFA CHAMPIONS LIGI, LEO Jumanne na Jumatano Usiku zitakuwa na Mechi zake za Kwanza za Nusu Fainali huko Jijini Madrid Nchini Spain.
LEO Jumanne, ndani ya Estadio Vicente Calderon, Vinara wa La Liga, Atletico Madrid, wataikaribisha Chelsea ya Engand.
Siku ya Pili yake, yaani Jumatano Usiku, huko Santiago Bernabaeu, Real Madrid watakuwa Wenyeji wa Mabingwa Watetezi wa UCL, Bayern Munich.



ATLETICO MADRID v CHELSEA:
Jose Mourinho ameshawahi kuifikisha Chelsea mara 2 Nusu Fainali ya UCL, Mwaka 2005 na 2007, na kutolewa na Liverpool.

Lakini safari hii wapo Uwanja wa Vicente Calderon ambao Atletico Madrid hawajafungwa hata Mechi moja ya La Liga Msimu huu na wanaongoza Ligi hiyo ya Spain wakiwa Pointi 4 mbele ya Barcelona.
Chelsea watatinga kwenye Mechi hii bila ya Fulbeki wao Branislav Ivanovic ambae amefungiwa na hili linaweza kumrudisha Kikosini Mkongwe Ashley Cole ambae amepoteza namba kwa Cesar Azpilicueta ambae atapelekwa Fulbeki ya Kulia na Cole kucheza kushoto.

0 maoni:

Post a Comment

waliotembelea blog