Tuesday, April 22, 2014



Hatimaye kocha Manchester United David Moyes amefukuzwa kazi, miezi 10 baada ya kumrithi Sir Alex Ferguson.
United jana waligoma kuthibitisha kuhusu ripoti kwamba Moyes angefukuzwa mwishoni mwa msimu.
Moyes, 50, alichaguliwa na Sir Alex Ferguson kumrithi wakati kocha huyo mwenye 72, alipoamua kustaafu baada ya miaka 26 mwaka jana baada ya ligi kuisha.
Moyes aliondoka Everton na kusaini mkataba wa miaka sita na mabingwa ya Premier league.
Kwenye taarifa rasmi, klabu ilisema: “Tungependa kumshukuru kwa kazi nzuri aliyoifanya, uaminifu wake aliokuwa nao kwenye kazi yake”.
Ryan Giggs kwa pamoja na Nicky Butt watashika majukumu ya ukocha mpaka mwishoni mwa msimu.

Mashabiki wa United wakiwa wachache Uwanjani wakati wa malumbano ya hapa na pale kabla ya mtanange huku wakishinikiza baongo la  'Chosen One' kuondolewa uwanjani hapo..

Moyes akiwa amebeba kombe la Ngao ya Jamii (Community Shield) baada ya Man  United kuifunga Wigan bao 2-0 kwenye uwanja wa  Wembley mwezi wa Nane kipindi cha nyuma.

0 maoni:

Post a Comment

waliotembelea blog