Vijana
wakiwa kwenye matembezi ya Uzalendo yalioratibiwa na Umoja wa Vijana wa
CCM katika kuadhimisha miaka 50 ya Muungano ambapo vijana hao walianzia
matembezi kutoka ofisi za Mkuu wa Wilaya ya Temeke mpaka kwenye viwanja
vya sabasaba na kulakiwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Dk.Jakaya Mrisho Kikwete.
Rais wa
Serikali ya Mapinduzi Zanzibar Dk.Ali Mohamed Shein akizungumza na
Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Dar es salaam Ndugu Ramadhani Madabida muda
mchache kabla ya kupokea matembezi ya Uzalendo yaliofanywa na vijana
mbali mbali .
Rais wa
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk.Jakaya Mrisho Kikwete akiwa
ameshikilia picha ya Baba wa Taifa Mwalimu Julius Kambarage huku Rais
wa Mapinduzi ya Zanzibar Dk.Ali Mohamed Shein akiwa ameshikilia picha
ya Rais wa kwanza wa Zanzibar Sheikh Abeid Amani Karume baada ya
kuzipokea kutoka kwa vijana waliofanya matembezi ya Uzalendo.
0 maoni:
Post a Comment