Friday, July 17, 2015


MABINGWA wa Italy Juventus wamesisitiza Kiungo wao Paul Pogba hauzwi licha ya Ofa kutoka Barcelona.
Joan Laporta, Rais wa zamani wa Barca ambae sasa anagombea tena nafasi hiyo, ameweka kwenye ajenda yake kuwa akichaguliwa Urais basi atamnunua Pogba.
Laporta yupo kwenye kinyang'anyiro cha kugombea Urais pamoja na Rais wa sasa Josep Maria Bartomeu, August Benedito na Toni Freixa.
Pogba, Kijana wa Miaka 22 wa Kifaransa alietokea Man United kwenda Juve, pia anawindwa na Manchester City na Chelsea.
Mkurugenzi wa Juve, Giuseppe Marotta, amesema: "Yeyote anaemtaka Pogba anapaswa kuongea na sisi na si Wakala Mino Raiola. "

Aliongeza: "Tumezungumza na Barca katika Miezi ya hivi karibuni lakini hauzwi. "
Hata hivyo, hata kama Barca watamnunua Pogba ambae ana Mkataba hadi 2019, hawawezi kumtumia hadi Januari 2016 kutokana na kufungiwa na FIFA kwa kukiuka Kanuni za Usajili wa Wachezaji Chipukizi.
Licha ya Adhabu hiyo, Barca imeshasaini Wachezaji Wawili katika Kipindi hiki cha Uhamisho ambao ni Aleix Vidal kutoka Sevilla na Kiungo wa Uturuki anaetokea Klabu ya Atletico Madrid Arda Turan.

0 maoni:

Post a Comment

waliotembelea blog