Monday, September 21, 2015


Mgombea urais wa Tbanzania kupitia CCM, Dk John Magufuli akiwapungia mkono wananchi wakati wa mkutano wa kampeni za urais, ubunge na udiwani kwenye Uwanja wa Michezo mjini Chato, mkoani Geita, jimbo alilokuwa Mbunge. Pia alitumia fursa hiyo kuwaaga wapiga kura wake.Mkutano huo wa kampeni ulijaza watu kupita kiasi  jambo ambalo wenyeji wa wilaya hiyo pamoja na mgombea amesema haijawahi kutokea.PICHA ZOTE NA RICHARD BMWAIKENDA;KAMANDA WA MATUKIO BLOG
Mbuzi huyu aliyechorwa maandishi hayo aliletwa kwenye mkutano huo na mmoja wa wafuasi wa CCM kwa lengo la kuwakebehi Ukawa.
Dk. Magufuli akijinadi kwa wananchi wa Wilaya ya Chato ili wampigie kura nyingi yeye pamoja na mbunge na diwani wa CCM.
Dk Magufuli akiwahidi wananchi kuwa akipewa ridhaa ya kuongoza nchi atahakikisha  elimu ya bure inatolewa kuanzia shule za msingi hadi kidato cha nne Mke wa  Mgombea urais wa Tganzania kupitia CCM, Janeth Magufuli akipongezwa na mumewe, Dk Magufuli baada ya kutoka kumuombea kura 
Wasanii wa muziki wa kizazi kipya wakitumbuiza wakati wa mkutano huo
Baadhi ya wananchi wakiwa na mabango yenye ujumbe tofauti
Baadhi ya wapigapicha za habari wakiwa juu ya magari kwa lengo la kupata picha nzuri wakati msafara wa Dk Magufuli ulipokuwa ukitokea nyumbani kwao kwenda kwenye mkutano wa kampeni kwenye Uwanja wa Michezo mjini Chato leo
Dk Magufuli akiingia kwenye mkutano wa kampeni mjini Chato   Kikundi cha ngoma za asili cha Mchele Mchele kikitumbuiza katika mkutano huo
Wanamuziki wa Yamoto Band wakitumbuiza  wakati wa mkutano huo
Wafuasi wa CCM wakionesha dole gumba ikiwa ni ishara ya kumkubali Dk Magufuli kuwa rais
Msanii Khadija Kopa wa Kikundi cha Sanaa cha CCM cha TOT, AKITUMBUIZA KWA WIMBO WA TAARABU WAKATI WA KAMPENI HIZO
Wasanii wengine wakiendelea kuunga mkono Malkia wa Mipasho Khadija Kopa
Mjumbe wa Kamati ya Kampeni za CCM, Abdallah Bulembo akielezea wasifu wa Dk. Magufuli uliomfanya ateuliwe na CCM kuwa mgombea urais wa Jamhuri ya Tanzania.
Dk Magufuli akizungumza na Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Geita, Josph Musukuma wakati wa kampeni hizo
Mwakilishi wa watu wenye ulemavu wana CCM na wasio wanaCCM, Amon Mpanju akihutubia kwa kuelezea ubaya wa Ukawa na kusifia CCM ambayo alidai inawajali walemavu nchini.

0 maoni:

Post a Comment

waliotembelea blog