Monday, September 21, 2015


Anthony Martial Mechi yake ya kwanza tu ya Ligi Kuu England ambayo alianza tangu mwanzo, Amefunga Bao 2 wakati Manchester United inaicharaza Southampaton Bao 3-2 katika Mechi ya Jumapili ya Ligi Kuu England huko Saint Mary.
Mechi yake ya kwanza kabisa ya Ligi kwa Martial, Kijana wa Kifaransa wa Miaka 19 tu, ilikuwa huko Old Trafford hapo Septemba 12 ambapo aliingizwa toka Benchi na kupachika Bao murua wakati Man United inaitandika Liverpool 3-1.
Hapo Jana, huku Man United wakiwa Bao 1-0 nyuma walipocheza na Southampton, Martial, akicheza Sentafowadi, huku Kepteni Wayne Rooney akiwa nyuma yake, ndie aliesawazisha Bao na kisha kupiga Bao la pili na Man United kwenda Bao 2-1 mbele.
Bao la 3 la Man United lilifungwa na Juan Mata wakati Bao zote za Southampton zikifungwa na Graziano Pelle.
Akimwongelea Martial, Mchezaji wa zamani wa Southampton, Morgan Schneiderlin, ambae Jana alirejea Saint Mary kuikabili Timu yake ya zamani kwa mara ya kwanza, alisema: “Kama mlivyomwona, ni mtulivu, hana mchecheto. Ana kipaji kikubwa. Amekuja Ligi Kuu England na anafunga. Ni Mchezaji mwenye akili mno, alietulia. Atakuwa Mchezaji Bora mno kwa Man United!”
Nae Meneja wa Man United, Louis van Gaal, ameeleza: “Ni kweli ameanza vizuri lakini tatizo ana Miaka 19 tu na usitegemee kila Siku atacheza vyema lakini amecheza Mechi 3 mfululizo kwa kiwango cha juu na kufunga Mabao, na hilo ni muhimu!”
Jumatano Man United ipo Old Trafford kucheza Mechi ya Raundi ya 3 ya Capital One Cup dhidi ya Ipswich Town na Jumamosi ijayo wapo tena Old Trafford kuivaa Sunderland kwenye Mechi ya Ligi Kuu England.
Huenda Mashabiki, ambao sasa wameanza kuwakebehi wapinzani walipochekwa kwa Bei mbaya aliyonunuliwa Martial, wakaendelea kujigamba.

0 maoni:

Post a Comment

waliotembelea blog