KOCHA wa Netherlands Louis van
Gaal ametoboa kuwa alipata shida sana kumpata Mchezaji wa kupiga Penati
ya Kwanza ilipofikia hatua ya Mikwaju ya Penati Tano Tano baada Timu
yake na Argentina kutoka 0-0 katika Dakika 120 za Nusu Fainali ya Kombe
la Dunia hapo Jana.
Kwenye Penati hizo, Argentina waliibuka kidedea kwa kushinda Penati 4-2 baada Holland kukosa Penati mbili zilizopigwa na Ron Vlaar na Wesley Sneijder na Kipa Sergio Romero kuokoa.
Beki Ron Vlaara ndie aliepiga Penati ya Kwanza.
Lakini Louis van Gaal, ambae Timu yake iliitoa kwenye Robo Fainali Costa Rica kwa Penati ambazo mbili kati yake ziliokolewa na Kipa wa Akiba Tim Krul alieingizwa Dakika za Mwishoni kwa ajili tu ya Penati, Jana alishindwa kutumia mbinu hiyo hiyo baada ya kuwa tayari washabadilisha Wachezaji Watatu.Akiongea na Wanahabari mara baada ya Mechi, Van Gaal alisema: “Ile na Costa Rica ingetupa imani kwani tulipiga vizuri sana. Lakini tatizo lilikuwa nani apige ya kwanza na niliwaomba Wachezaji Wawili na mwishoe nikaangukia kwa Vlaar. Yeye ndie alikuwa Mchezaji bora hivyo angekuwa anajiamini mno. Lakini hii inaonyesha jinsi ilivyokuwa ngumu kupiga Penati kwenye Penati Tano Tano.”
Aliongeza: “Ni mbaya mno, kupoteza Mechi kwa Penati. Ukiondoa yote, tulikuwa sawa na wao, kama sio Timu bora. Inahuzunisha sana!”
Messi akifunga penati

Kwenye Mikwaju Mitano ya Penati, Lionel
Messi alianza kuifungia Argentina na Ron Vlaar kukosa kwa Netherland
baada Kipa kuokoa, kisha Arjen Robben akafunga na Ezequiel Garay kuipa
Argentina 2-1.
Sergio Romeo akiokoa mkwajuWesley Sneijder alikosa penati...!
Maxi alifunga penati..

Akaja Wesley Sneijder na kukosa kwa Kipa kuokoa huku Sergio Aguero akifunga na Argentina kuwa 3-1 mbele.
Dirk Kuyt akafunga kwa Netherlands na kuwa 3-2 lakini Maxi Rodriguez akapiga Penati ya 4 na Argentuna kushinda 4-2.Maxi akishangilia penati aliyofungaFuraha kwa Wachezaji wa Argentina baada ya kufunga mikwaju ya penatiKipa wa Netherlands hoi!!!

0 maoni:
Post a Comment