Thursday, July 10, 2014


NIGERIA imesimamishwa na FIFA baada ya Shirikisho la Soka la Nigeria, NFF, kuingiliwa shughuli zake.
Hii Leo FIFA imetoa taarifa kwamba Kamati ya Dharura imeamua kuisimamisha Nigeria mara moja baada Mahakama Kuu ya Jos, Plateau State, kusimamisha shughuli za NFF na kumtaka Waziri wa Michezo wa Nigeria kumteua Mtu kuendesha shughuli za NFF.
FIFA imesema maamuzi hayo ni kinyume na Kanuni ya 13, Aya ya 1 na Kanuni ya 17, Aya ya 1 ya Sheria za FIFA ambazo zinataka Vyama vya Wanachama wake kuendeshwa huru na kutoingiliwa na upande mwingine wowote.

Hapo Julai 4, Katibu Mkuu wa FIFA, Jerome Valcke, aliiandikia Nigeria na kuipa hadi Julai 8 kuirudisha Madarakani NFF na kutoingiliwa tena kwa namna yeyote.
Barua ya Valcke iliikumbusha Nigeria wajibu wake wa kuiruhusu NFF kuendesha shughuli zake bila kuingiliwa na Mtu yeyote kwa mujibu wa Kanuni ya 13 ya Sheria za FIFA.
Pia Barua hiyo iliionya Nigeria kuwa endapo NFF haitarejeshwa madarakani ifikapo Julai 8 basi Vyombo husika vya FIFA vitachukua hatua zaidi ikiwa pamoja na kuisimamisha Nchi hiyo kwenye shughuli zote za Kimataifa za Soka ikimaanisha kufungiwa kwa Timu yao ya Taifa na Klabu zao zote kucheza michuano ya Kimataifa.
Uamuzi huu wa Leo utaifaya Nigeria isiweze kushiriki Mashindano yeyote ya Kimataifa.

0 maoni:

Post a Comment

waliotembelea blog